Jumatatu, Julai 18, 2011

Mke wangu anatumia muda mwingi na marafiki zake nyumbani hatulii,,tabia hii imenichosha.

Mimi  ni mwanamume nina mke na watoto watatu naipenda sana familia yangu, Mimi nafanya kazi na katika kazi ninayoifanya huwa natoka saa kumi na mbili jioni na hupendelea kurudi nyumbani mapema tatizo lipo kwa mke wangu ambaye huwa anatoka kazini mapema lakini anachelewa kurudi nyumbani wakati mwingi hurudi saa sita za usiku na mimi ndiye ninayemfungulia mlango nilishawahi kuzungumza naye juu ya tabia yake lakini hakunisikkiliza na muda huo anautumia kuwa na mashoga zake tena wanakaa bar huku wakinywa pombe yaani hana muda na watoto tabia hii inanikera sana na bado napata maneno mengi sana yanayomuhusu yeye kuwa anamahusiano nje inaniuma sana nimeshajaribu kumbadilisha imeshindikakana sasa natamani tuachane lakini nawafikiria sana watoto wangu sijui nifanyeje...


Jamani hii ni tabia ya baadhi ya wanawake ambao hawajatulia katika ndoa zao inawezekana ni tabia yake tokea mwanzo,,au marafiki alionao ndiyo chanzo, inasikitisha sana kwanini mwanamke usitulie na kuilea familia yako kwa mapenzi na amani ushauri wenu wadau..........

Maoni 6 :

Bila jina alisema ...

pole sana kaka huyo mama hajatulia jaribu kumuelimisha ikishindikana achana naye hajatulia

Bila jina alisema ...

khaaa mwanamke kuwa na tabia kama hizo haipendezi kabisa

Bila jina alisema ...

naitwa Lina huyo mama ajiheshimu inawezekana ana bwana anamchanganya huko nje mpe talaka akajifunze adabu

Bila jina alisema ...

Mwache huyo atajijua huko mbeleni.Mwanamke ndiyo ndoa bwana tena iweje huyo wako afanya vituko hivyo wakati wanawake wengi ndo wanalalamika waume zao kuwa na tabia hiyo tete.

Bila jina alisema ...

Sasa kama utawahurumia watoto kwa kuendelea na mwanamke ambae atakuletea maradhi ambayo yatasababisha...MFE NYOTE NA MUWACHE WATOTO KWENYE MATESO HAYO AMBAYO UNAYAHOFIA SASA HIVI......NI BORA UKAMUACHA ILI UWE AFYA YAKO NJEMA UWEZE KUWALEA WATOTO, KULIKO KUENDELEA KUISHI NA HUYO MWANAMKE...MPE TALAKA...

Bila jina alisema ...

Ndugu kama una mapenzi na wanao nakushauri umuache mkeo haraka sana kwani mtakufa na kuwaacha hao watoto unaowapenda yatima. Ni mara kumi walelewe na mama wa kambo kuliko kuwa yatima na omba omba kwenye nyumba za ndugu zako. Mimi nina mfano hai wa jirani yetu, nimepata taharifa kuwa mkewe amefariki (mi niko nje ya nchi) Lakini huyo mama alikuwa ni bad news na watu walikuwa hawamuelewi mumewe inakuwaje anakaa na mke malaya. Sasa na mume anasubiri tarehe tena ni baba msomi engineer. Watoto sijuhi nani atawalea maana ni wadogo. Chukua maamuzi haraka sikutishi; mtu mzima afundishwi tabia.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom