Jumatano, Julai 27, 2011

Ni namna gani unaweza kulinda uaminifu katika mahusiano ya kimapenzi "

Dk. Paul Nelson wa Kliniki ya afya ya mapenzi kutoka jijini Mwanza akiwa na mtangazaji wa Passion fm Anneth Nyoni katika kipindi cha The Big Show ambapo amezungumzia namna ambavyo mtu anaweza kulinda uaminifu katika mahusiano ya kimapenzi, Katika mahusiano ili kulinda uaminifu ni muhimu kujitambua na kumtambua mwenza wako katika mambo mbalimbali likiwemo suala la kuwa muwazi kwenye kila eneo.

Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya watu kuona kwamba uaminifu upo kwenye tendo la ndoa pekee kwa mfano usaliti wa mapenzi lakini ikumbukwe kwamba uaminifu unaangalia sehemu nyingi likiwemo suala la umiliki wa mali,kuzingatia ahadi, kutokuwa muongo, nk. Hivyo ni muhimu kulinda uaminifu ili kuwa na uhusiano ulio na furaha wakati wote.

Pichani ni kitabu kilichoandikwa na Dk. Paul Nelson kinaeleze masuala mbalimbali ya kimapenzi likiwemo suala zima la uaminifu kinapatika mitaani hivi sasa kwa gharama ya shilingi 5000 za kitanzania

kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Dk.Nelson kupitia 0754039994  au barua pepe kumbatiapenzi@yahoo.com

Maoni 4 :

Bila jina alisema ...

nakitafuta sana hicho kitabu

Bila jina alisema ...

uaminifu ni kila kitu katika mahusiano nahitaji hicho kitabu

Bila jina alisema ...

I think this is one of the most important information for me. And i am glad reading your article. But should remark on few general things, The website style is perfect, the articles is really nice

Simon Kitururu alisema ...

Tukumbuke pia BINADAMU ni kiumbe complicated. Si kila kifanyacho kazi kwa mwenzio kitafanya kazi kwako hata kama hicho ni jinsi ya kuchezea kiharage.

Kwa hiyo kumbuka WEWE ni wewe na soma vitabu hasa vya ushauri huku ukijikumbuka kuwa labda utafiti wa kitabu hicho haukufanywa kwa kuzingatia yako na au tu WEWE!

Nawaza tu kwa sauti!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom