Jumatano, Julai 27, 2011

Utajuaje kama mwenza uliyenaye anakupenda??

Katika mahusiano ya kimapenzi mara kwa mara watu wengi wamekuwa wakijiuliza maswali haya je mwenza wangu kweli ananipenda? Je mimi mwenyewe nampenda? haya ni maswali ambayo hutoka moja kwa moja moyoni na majibu yake tunayo sisi wenyewe, mara nyingi kwenye mahusiano watu hujisahau kujitambua wenyewe  na hivyo kupelekea tushindwe kujielewa na kujibu maswali yanayotuhusu kuhusu mapenzi au upendo,

Hakuna jambo zuri katika uhusiano kama  kutambua kuwa mwenza wako anakupenda au wewe mwenyewe unampenda bila kuwa na kificho, utani bali ni ukweli mtupu ukweli huo ni kama mwenza wako yupo tayari kufa kwa ajili yako au wewe upo tayari na katika kusema kufa si kwamba kuwa mjiue kwa pamoja bali ni ule uwezo wa  upendo wenu katika kulindana na kufanyiana mambo ambayo yatawafurahisha wote huo ndiyo upendo wa dhati,

Upendo ni  ule ambao unakuja wenyewe unajikuta unamfanyia mwenza wako mambo makubwa kuliko yeye au yeye anakufanyia mambo makubwa kuliko wewe huo ndio upendo na hata siku moja hauwi sawa pande zote, vilevile mtu anayekupenda ni yule ambaye yuko tayari kukusaidia na kujitolea kwa kuonesha upendo wake kwako bila ya choyo na tena kwa vitendo na hata kama kuna tatizo wapenzi walio katika mapenzi ya kweli basi hutumia njia ya mawasiliano yaliyo bora katika kuzungumza na kutatua matatizo hayo. Upendo mzuri ni wa kutoka moyoni pekee jitambue na umtambue anayekupenda

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom