Jumatatu, Julai 04, 2011

Nikiwa napesa mapenzi yanakuwa motomoto,,nikiwa sina kila siku tunagombana

Mimi ni mwanamume nipo katika mahusiano na mpenzi wangu ninaye mpenda sana na matarajio yangu nikuja kufunga naye ndoa hapo baadaye mwanzoni wa uhusiano wetu  mpenzi wangu alinikuta nikiwa na uwezo kifedha hivyo nilikuwa nikimpa kila kitu anachohitaji na wakati huo mapenzi yalikuwa motomoto kwani alikuwa akinipenda sana lakini ilifika kipindi hali yangu kifedha ilikuwa si nzuri niliona tabia ya mpenzi wangu imebadilika kwani hata nilipokuwa namuhitaji alikuwa hana muda na mimi na wakati mwingine alikuwa anazungumza maneno yanayonitatiza alishawahi kuniambia kuwa hapendi mwanamume akiwa hana hela,,nilijaribu kumuelewesha  kuwa  pesa haitabiriki leo unaweza kuwa nazo kesho usiwe nazo,,

Hali hiyo  iliendelea kiasi kwamba ikawa kama tumeachana hivi sasa mambo yamebadilika nimeanza kupata fedha mpenzi wangu amerudi na kuniomba msamaha huku akisema kuwa ananipenda sana mimi binafsi bado nampenda lakini na wasiwasi huyu mwanamke anaweza kubadilika tena nikiwa sina pesa..KUWA MAKINI KATIKA KUCHAGUA MPENZI WENGI WAPO KWAAJILI YA MASLAHI NA SIYO MAPENZI...

Maoni 7 :

Bila jina alisema ...

POLE ILA HUYO MWANAMKE CYO KABISA HAKUPENDI YUPO KIHELA ZAIDI SO KAZI KWAKO KUENDELEA NAYE AU KUMUACHA MANA MUNGU KISHAKUONESHA KWAMBA CYO MKE HUYO.

Rik Kilasi alisema ...

SASA WEWE KWA AKILI YAKO UNADHANI KUNA MWANAMKE WA KUOA HAPO? MBONA LIKO WAZI KAMA MTU KAKUACHA KISA HUNA PESA NA SASA ZIMERUDI NAYEYE ANARUDI HUYO NI MWIZI NA MUIGIZAJI WA MAPENZI, NA MUDA HUO LAZIMI ALIKUA ANA DATE MTU MWINGINE ANGALIA BRO MAGONJWA MENGI SASAHV

KIFUPI HUHITAJI KUFIKIRIA SANA HUYO ACHIA WENYE PESA NO WONDER HATA MARA YA KWANZA ULI LOST KWAAJILI YAKE MBONA WANAWAKE WAPO WENGI TU KAKA, YAANI YEYE AKIKUONA ANAONA PESA WEWE NI KAMA KIVULI TU NA KAMA UNATAKA KUISHI MAISHA YA PRESHA NA KUZEEKA HARAKA OA HUYO DADA.

NB:HUO NI MTAZAMO WANGU SI LAZIMA KUUFUATA!!

Bila jina alisema ...

hana lolote huyo ni tapeli wa mapenzi usikubali kurudiana naye

Bila jina alisema ...

kaka yaani hilo lipo wazi huyo mwanamke ukiishiwa lazima akuache kuwa makini watu sikuhizi wapo kimaslahi zaidi naitwa Rozi

Bila jina alisema ...

naitwa Baba July haya mambo yapo sana jamani wanawake wa siku hizi unashindwa kumuelewa amekupenda au anapenda pesa zako

Bila jina alisema ...

dude jaribu kua creative... kama anasema anakupenda jaribu kum test tena na ilo ilo swala la hela. mpe jaribio la miezi miwili. kila ukiwa uko nae mwonyeshe huna hela hata kama unayo. kua mvumilivu kaka katika zoezi hili..mpe miezi miwili tu utajua uko na mke au box....

Hansmas alisema ...

wanawake wa leo wako kimaslahi zaidi, yaani hapo kaka unaliwa tu hakuna love. Jifunge mkanda ufanye jaribio tena la makusudi tena safari hii jichokeshe kabisa.... vaa hadi vilaka halafu majibu utayapata....

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom