Jumatano, Julai 06, 2011

Wanaume au wavulana siku hizi hawataki kutegemewa kwa kila kitu ni vizuri mwanamke kuepuka kuwa tegemezi.

Ni wazi kabisa kwa asilimia kubwa ya wanaume sikuhizi hawataki kutegemewa kwa kila kitu kwani maisha yamekuwa magumu wakati mwingine unakuta hata wao wenyewe wanashindwa kujitosheleza hivyo kuwa na mpenzi tegemezi wanaona ni hasara  kubwa na kutokana na hilo mwanamume akiona mwanamke pale mwanzo tu baada ya kumtokea mara anaomba vocha, msaada wa kifedha yaani shida zako zote unataka mwanamume akusaidie kiukweli si kitu kizuri ndiyo maana baadhi ya wanaume wakiona tabia kama hizi basi anaanza kukata mawasiliano taratibu mwishowe ukimpigia simu hapokei kabisa .

  Ni muhimu kujituma ili usiwe ombaomba kila wakati kwani inawezekana mwanamume akakuchoka kutokana na wewe kila wakati kutaka pesa, ijapokuwa wapo baadhi ya wanaume wana huruma na wako tayari kukusaidia kwa lolote ambalo lipo ndani ya uwezo wake hata kama hana uwezo mkubwa kifedha pamoja na hayo usiwe tegemezi fanya kazi kwa bidii ili hata ikitokea na yeye anahitaji msaada wako basi unamsaidia. na hili ni kwa wote mwanamke na mwanamume tushirikiane na si kumuacha mmoja aumie zaidi.

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

hawawezi kukwepa coz wameumbiwa hivyo, kula kwa jasho toka kuumbwa kwa ulimwengu.

Susan Wamunza alisema ...

Ni kweli dunia ya sasa kumtegemea mwanaume pekee nayo tabu ila wanaume wanatabia mbaya akiona unamsaidia kwenye baadhi ya mambo basi anadhan unampenda kuliko maelezo ataanza kukunyanyasa ndio mana tunaona bora wafanye wenyewe tu mana ndivyo mungu alivyosema.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom