Jumamosi, Agosti 27, 2011

Mimi ni mwanamume naombeni ushauri mke wangu hapendi tuishi nyumbani kwa wazazi wangu,,

Habari yako Adela naomba ushauri kupitia blog yako mimi ni mwanamume nina mke na mtoto mmoja, ambao ninaishi nao nyumbani kwa wazazi wangu nikiwa kama mtoto wa kwanza katika familia wazazi wangu wananitegemea na pia hawapendi mimi niishi mbali na nyumbani, binafsi nimekubaliana nao lakini tatizo linakuja kwa mke wangu hataki tuendelee kuishi na wazazi nimekuwa nikimkatalia lakini kila kukicha ananisisitiza na sababu anasema ili kuepusha ugomvi wa familia hadi hivi sasa tuna ugomvi mimi na mke wangu kutokana na hili mimi nahisi hawapendi ndugu zangu naombeni ushauri wenu

Maoni 13 :

Bila jina alisema ...

Kuishi na wakwe kazi. Na hasa mamamkwe na masister wa mume. Mie nampa sifa njema mkeo kwa kuvumilia muda wote mpaka sasa.

Mie nazani kuna vitu anajaribu kuviepuka hapo,ndio maana anataka kuama.

Mwisho baada ya mwisho atakuambia amechoka, na atadai talaka yake.


UKWELI NI KWAMBA
Mama wakwe na ma wifi wao kazi yao ni kucritisize mke wa kaka, mke wa mtoto wao.

Akiuguza chakula kwa bahati mbaya, Asubuhi majirani wote wamesha ambiwa, (mama nani kaunguza chakula jana).

Mtaa mzima unajua huyo mama anii anavo safisha nguo, vyombo na mpaka anavo mlisha mwanae nk.

Mabaya yote upande wake wanaweka uwanjani kila mtu ayaone, ili kumuaibisha, na mazuri wanayaficha uvunguni.

MWANAMKE
Sie wanawake tunaogopa wakwe siku ukikosea kitu kidogo tu, maneno mpaka watu wote wanao kuja wanaambiwa. TUNATIWA AIBU.

Na tunaogopa kufanywa watumwa wa waume zetu, tuwafanyie kazi mamamkwe, babamkwe, masister na ma brother wa waume zetu, khaa maisha gani hayo?

Hata kule kijijini watu uishi karibu na wazazi ila kila mtu na kibanda chake ili kuepusha kusemana semana, na kutumikishana.


Jua, unaweza kuishi karibu na wazazi wako ila kila mtu na nyumba yake. Wewe na mkeo munaweza kupanga jinsi ya kuwaelewesha na kuwalidhisha kuama kwenu, kwa mfano munawambia wazazi kwamba munaitaji uhuru wa kuwa peke yenu kwa sasa. Na kuwa hakikishia mkeo anaweza kwenda mara kwa mara kuwajulia hali na kuwasaidia kazi za nyumbani.

Nazani wazazi wako hawato lalamika.
Na wakilalamika basi wazazi wako ndio hawampendi huyo mkeo.


Kabla sijaendelea ningependa kujua, hao wazazi wako wazee kiasi gani? wazee sana? Hawawezi kujifanyia vitu vyao wenyewe kabisa? hawawezi kujitegemea? na ndugu zako wakike wangapi na wa kiume wangapi na wote wanaumri gani na kazi gani? na wewe una umri gani na kazi gani?
munaishi wapi na munaishije? mupo wangapi ktk nyumba?

Hii itanisaidia kupata picha ya familia yako na jinsi ya kuchangia wazo.

Hata hivo nakupa pole, mie najua family problems. upo katika dilemma

Bila jina alisema ...

inawezekana mkeo akawa sahihi kwani hata ukiishi mbali na wazazi si utawasaidia tu minaona ni bora uishi nyumba tofauti na wazazi inaleta heshima zaidi

Bila jina alisema ...

mdau hapo juu mimi ndiye niliyeomba ushauri hawa wazazi wangu ni watu wazima mama ana miaka karibia 55 na baba 62 hapo nyumbani naishi pia na wadogo zangu lakini ni familia nzuri tu iliyojaa upendo pamoja na hayo mke wangu anachotaka mimi na yeye tukaanzishe mji wetu.

Bila jina alisema ...

Nimerudi tena.

Mie naona mkeo anakushauri kitu cha akili sana. Kama familia yako ni nzuri na ilio jaa upendo, basi watakuelewa utakapo waambia unampango wa kuanzisha mji kwa ajiri ya wajukuu zao.


Kama wazazi wako wanaupendo watakuruhusu tu kwa heri na baraka tele. Na kukutakia ufanikiwe hizo plan zenu.

Mie kwa mtazamo wangu mama wa miaka 55 sio mzee na hata baba wa miaka 62bado ananguvu zake. Kama wazima tu kiafya, wanaweza kujishughulisha kidogo kidogo. Ingekuwa wanamiaka 75-80 hapo ningechangia ukae nao nyumba moja maana ni wazee. Na hisitoshe wadogo zako wapo hapo hapo nyumbani hawato jisikia wapweke, kuna ubaya gani wewe kuwafamisha unaenda kujenga mji. Na wakikulaumu basi watakuwa hawakutaki mema wewe na wala kizazi chako.



Jua ingawa wewe ni wa kwanza, lakini mzigo sio wako peke yako. Jukumu lenu wote, hata ndugu zako wanajua wao wanajukumu lao kwa wazazi wao pia. Ila wewe ni kiongozi wa kujua musaidie vipi wazazi wenu.

Na wazazi wakisha kufariki hao hao nduguzo pengine wakakubadirikia, wengine watadai nyumba iuzwe mugawane mali.

Na kusababisha muonane wabaya na watoto wenu wasipendane.

Mkeo kasha yaona hayo yatakayo kuja, musije kumbuka hapo baadae.

Nendeni huko mukaunde mji wenu, ya wazazi na wadogo hachana nao, angalia future na kujiendeleza. Ila kuwasaidia na kuwa nao karibu mara kwa mara ni kitu muhimu. Au wewe mwenyewe umewazaje? umeplan nini maishai mwako? umeplan uishi home ya wazazi mpaka uzeeni kwako?

Bila jina alisema ...

JIANDAE KUKOSA MKE. KWANZA MAMA YAKO NI KIJANA SANA. MAMA YANGU MIE ANAMIAKA 70 NA ANACHAPA KAZI KAMA KAWAIDA. NA ANAENDELEA KULEA WAJUKUU ZAKE 4, PEKE YAKE. BABA YETU KAFARIKI MWAKA JUZI MIAKA 78, HADI KAFA AKIJITAFTIA RIZKI MWENYEWE. MJUKUU WAKE WA KWANZA ANA MIAKA 25 NA KASHA ZAA PIA.

HAO WAZAZI WAKO WANAUPUNGUFU GANI? NINACHOKUSHAURI KAMA WAMESTAFU BASI WASHAURI WASIKAE HOME TU BILA KUFANYA KITU, SIO NZURI KWA AFYA. WAFUNGULIE MGAHAWA, AU WAFUNGULIE KADUKA ILI WAWE NA HOBBY YA KUFANYA NA KUINGIZA CHOCHOTE KITU KIWASAIDIE. AU KAWATAFTIE SHAMBA AU GARDEN, WAPANDE VEGETABLES, WAUZE. AU WAPANDE MAHINDI WAUZE WAPATE ELA ZIWASAIDIE, WANAWEZA KULIMISHA WATU PIA WAO WAKASIMAMIA TU.

WEWE KUWA TEGEMEZI WA NYUMBA MZIMA SIO VIZURI,WATAKUFUMUA HAO KAKA YANGU. NA UKIFA, WATAMTEGEMEA NANI? FAMILI ZINGINE AKILI MBOVU, SAMAHANO

Bila jina alisema ...

Wewe kaka ni dini gani? maana sisi wakristo tunajifunza katika maandiko kuwa "Mwanamume atamwacha baba na mama yake naye ataambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja..." kwa mtazamo sidhani kama kuna mwanamke anayependa aolewe then wakae ukweni, mi pia siwezi kukubali hilo hata kama hao wakwe wana upendo wa kiasi gani. Mambo ya familia ni magumu na ndoa si lele mama, ninyi mnaweza kuvumiliana ktk matatizo madogo madogo ktk ndoa, lkn si mtu mwingine, binadamu hatuishi kujikwaa, lkn si kila mtu anaweza kuchukuliana na makosa ya mtu mwingine, bali wanandoa wanaweza kuchukuliana ktk makosa si wakwe kwa mkwe wao awe wa kike au kiume. Au utuambie kaka hao wazazi ndo wafadhili ktk maisha yenu, kama sivyo, na ni kuwasaidia tu..unaweza kuwasaidia hata mngekuwa mnaishi nchi tofauti. Nampa hongera mkeo kwani ni mvumilivu, na anachosema ni haki yake...uking'ang'ania na msimamo wako subiri akukimbia..

Bila jina alisema ...

Unamnyima Mkeo Uhuru wa mama na nyumba yake, kaanzisheni mji wenu for the seek of your child pia. Angali na mbele maisha yatakuwaje kwa watoto na mkeo kama ukifa? wazee bado wana nguvu, hata ukiwa mbali utaweza kuwasaidia tu.
By Gilo

Bila jina alisema ...

nimeipenda hii wanaume huwa hawalioni hili wanakimbilia kusema eti hawapendi ndugu zangu hilo hapoa halihusu kabisa binti kaolewa na wewe mume na c na familia nzima hata kama mna upendo wa agape kila mtu akae kwake iwe ni kutembeleana.. jamani mi naishi na mkwe ni utata mtupu haitakuwa njema kuweka mapungufu yake hapa lkn amini ucamni ni kukwazika kwa kwenda mbele...

Bila jina alisema ...

Mkeo ana akili, hakuna baya na anakushauri vyema. Ukweni kwakweli hata kama wanampenda vipi huyo mkeo hamtakuwa na uhuru wa asilimia 100 ya kufanya mambo yenu ya kimaendeleo au hata ya unyumba.Kuna mambo mengine mkeo atashindwa kukufanyia ukiwa hapo kwa wazazi wako kwani ataona aibu mbele ya wakwe, shemeji na mawifi. Kwakweli even me I will not be confortable at all, mnakosa mengi kwa kukaa kwa wazazi wako. Maana huyo binti hata ile michezo ya "kinyani" ya mume na mke atakuwa anajilimit sana. Kuwa na mji wako, kwani hata wazazi wako nao walikuwa na wazazi na wakaanzisha mji wao. Mkeo anakushauri vizuri kwakweli, hameni tu!

Bila jina alisema ...

Uhame haraka unatuaibisha wanaume wenzako.Haiji akilini mtu mzima kama wewe umeoa na kuzaa mtoto bado unaona ni haki na bisara kukaa kwa wazazi wako.

Kama wazazi wanahitaji msaada wako basi nenda kapange karibu nao lakini siyo kuishi nyumba mwao.Ni aibu na ni mwiko kabisa kumleta mtoto wa watu nyumbani kwa wazazi wako.Unataka kumfundisha nini hapo?

Je, kama yeye atakuambia mkakae kwa wazazi wake utakubali?Kuamua kuoa maana yake umeamua kuanza maisha ya pekee ya kujitegemea pamoja na huyo unayeoana naye.

Kumbuka kuwa humpi heshima mkeo na uhuru wa kujitawala na kubuni mambo mapya kwa ajili ya kujenga familia na maendeleo ya kwenu.Ukitaka kuona mke wako anaugua rohoni ni hivyo unavyomfanyia.Hata kama familia yenu ni watu wazuri lakini haipasi muishi na mkeo kwenye nyumba hiyo.

Inaelekea ulioa kabla hujaamua na yamkinoi hujakua bado maana hujui nini maana ya kuwa na mke.Hata sijui unaonyesheje mapenzi kwa mkeo mbele ya wazazi wako? yaani umepewa chumba humo ndani na unakula nyapu kweupee humo ndani kwa wazazi.Unamnyima raha mkeo naamini hajawahi kufurahia mapenzi yenu tangu muoane kwa mazingira hayo.
Tafadhali hama haraka sana kabla maji hayajafika shingoni.Utamuua kwa mawazo mtoto wa watu.

Bila jina alisema ...

nimependa mawazo yenu hapo juu,,kwakweli kaka unatia aibu,na unamnyanyasa sn mkeo,,hama haraka hapo kwenu kaanze maisha yako,ha wazazi wako ni maselfish mbona wao walifanya maisha yao mkazaliwa nyie?kwann we watake kukufuga hapo?kweli hawakupendi naww huna akili wala msimamo wa maisha na ningekuwa mm wallah ningeshaomba talaka yangu ili ww upate uhuru wa kukaa na wazazi wako,,na ukiendelea kukaa hapo hutakuja kuendelea ht siku moja,mkeo ana akili sn na anahitaj pongezi kwanza kwa kuwa mvumilivu na pili kwa kukupa akili m hiyo inaelekea ww mtt wa mama kila kitu mpk mama ako akwambie ndo ufanye,,,na siku mama ako akisema umuache mkeo utafanya ivo,,hebu kua bwana unaaibisha wanaume wenzio,,km wazazi hawana msaidiz bas watafutie housegirl na uwe unawapelekea pesa za matumizi na siokumfanya mkeo ndo msaidiz wa familia yako unamshushia heshima yake kabisaa,,

Bila jina alisema ...

jamani watu woooooote mliyoyaongea ni sahihi inatia uchungu sana mke kukaa ukweni unakuwa kama yatima hata kama hao wakwe zako watakupenda kupitiliza bado unahitaji kukaa kwako binafsi huwezi kuwa huru.

Bila jina alisema ...

Jamani asanteni sana kwa ushauri wenu nimekaa nimetafakari ni kweli nahitaji kuanza maisha bila ya wazazi wangu na mimi niwe na mji wangu ila tatizo ni kwamba wazazi wangu hawajafurahia uamuzi niliouchukua kiasi kwamba inafikia hatua wanamchukia mkwe wao kwa kuhisi kuwa yeye ndiye kishawishi kikubwa

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom