Ijumaa, Septemba 23, 2011

Inawezekana ikawa ni rahisi ama ni vigumu kuwa na penzi la milele......


kuwa na penzi la milele ni ndoto za waliowengi katika mahusiano lakini katika mapenzi inawezekana ikawa ni rahisi sana kuwa na penzi la milele kama wawili wapendanao mmedhamiria kukabiliana na matatizo yote yatakayoweza kujitokeza baina yenu huku uaminifu ikiwa nguzo ya pekee kulinda penzi hilo, vilevile inaweza kuwa vigumu kuwa na penzi la milele kama ukikosekana uaminifu, uvumilivu, ubunifu na mambo mengine mazuri yanayoweza kuboresha penzi lenu wakati wote,,

MDAU UNASEMAJE KUHUSU ILI JE WEWE UNAONA NI RAHISI AU NI VIGUMU KUWA NA PENZI LA MILELE????


Maoni 1 :

Simon Kitururu alisema ...

Mie nafikiri BINADAMU kwakuwa anaudhaifu wa kibinadamu hili usemalo;

``katika mapenzi inawezekana ikawa ni rahisi sana kuwa na penzi la milele kama wawili wapendanao mmedhamiria kukabiliana na matatizo yote yatakayoweza kujitokeza ....´´


....HALIWEZEKANI kwa kuwa moja ya sifa ya BINADAMU ni kutojua ya mbeleni na ya mbeleni sidhani kama kuna MTU mwenye GARANTII kuwa ukiahidi milele -MILELE ni UWEZEKANO.


NA labda ikionekana MILELE au ukaendeleza ahadi MPAKA UFE haina maana unaendeleza kutii ahadi huku kweli AHADI IKO kiutamu VILEVILE.

Na nasikia ni wengi wako kwenye ndoa zilizokufa KWA KUFUATA USEMALO kwa kuwa waliahidi hii ndoa ni mpaka tufe ambacho ni sababu wanaishi na presha za mipaka ya kutunza yaheshimiwayo na jamii kwa kutunza hata MUONEKANO WA NDOA ingawa mapenzi yaliyofanya iwe ndoa YALIKUFA na maisha yashangiliwayo na watazamaji wa wapendanao ni kimuonekano tu.

Nanafikiri MTU ukianza kuhitaji ubunifu sana ili kutunza penzi,..
... labda penzi hilo lilishakwishnei.

Ndio mie naamini penzi la MILELE kwa binadamu zaidizaidi ni NDOTO ingawa labda ni kweli lawezekana kwa kuwa yasemekana MAMA ya MTU anaweza kupendwa tokea MTU azaliwe mpaka kwishnei.

Ni mtazamo tu huu!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom