Jumanne, Septemba 20, 2011

Nakosa raha kuishi nyumba moja na mke mwenzangu..

Habari yako Adela  pole na majukumu na hongera sana kwa blog yako nzuri, mimi ni mwanamke nimeolewa nina watoto watatu nikiwa mke wa kwanza kwa mume wangu nampenda sana kiasi kwamba aliponiambia kuwa anaoa mke wa pili nilimkatalia lakini kutokana na dini inaruhusu na yeye kuendelea kusisitiza baadaye ilinibidi nikubali kwani sikuwa na namna, sasa kinachoniumiza ni huyu mume wangu baada ya kuoa mke wa pili amemleta hapa nyumbani tunaishi naye ila vyumba tofauti nimejaribu kumuambia mume wangu anasema nina rohombaya na ubinafsi ukweli ni kwamba mwanamke aliyemuoa ni binti mdogo wakati mwingine kuna vitu tunapishana. 

Sijui nifanyeje hii hali mimi sijaipenda bora tungekaa mbalimbali,, naombeni ushauri wenu kwani mabadiliko ni mengi tangia mume wangu aoe mke wa pili wakati mwingine anadiriki kumsifia mke mwenzangu mbele yangu huku akinikandamiza mimi naumia sana sijui nifanyeje

Maoni 5 :

Bila jina alisema ...

masikini pole! huo ni ukatili wa hali ya juu, mwanaume kukuletea mke mwenzako na mkaishi nae nyumba moja. nachokushauri ndugu yangu just ignore him! jifanye kama humuoni, akija shukuru asipokuja shukuru! mungu ni mkubwa sana! first love is strong mamii, he will come back, lakini in the meantime ignore him!! kama unafanya kazi jikeep busy, kama hauna kazi dada ni stayhome mom ndugu yangu itakuumiza kwa muda mrefu, tafuta shughuli ya kufanya! utazoea, ila pole sana! huna la kufanya, mume unampenda! ilajamani sheria hizi nyingine zinamkandamiza mwanamke!

Bila jina alisema ...

yani wewe mwanaume ni bwege sana

Bila jina alisema ...

Nazani yeye mwanaume ndio mkatili, mnyanyasaji na mchawi, mwanga kakuloga.

Hachana nae, siku hizi hamna mapenzi ya kugawana we dada. Dini kitu gani? japo mie muislam ila siku mume wangu akiniambia anaongeza wa pili, mie natimua zangu. Naenda kujishia uko na watoto wangu, tena mbali na yeye, ili hasiniwangie.

Mwambie kwavile anakuona una roho mbaya, basi bora akupe talaka yako. Mwambie hauitajiki tena maishani mwake, na hata wewe haumuitaji tena.

mie nakuoneleni huruma sana nyie mnao nyanyasika na kujipendekeza kwa waume zenu, poleni.

Bila jina alisema ...

Kwa kweli no way...kwani dini inaruhusu mwanaume kuoa mke wa pili hata kama mke wa kwanza haridhii?
Huyo mume ni mbinafsi sana, ningekuwa mimi ningeachana nae kabisa maisha ni mafupi sana dadangu kwanini binadamu mwenzio akunyime raha hapa duniani?
Kama huna kazi tafuta hata biashara ujitegemee na uachane na huyo mwanaume hakuthamini wala hajali furaha yako, sasa wewe utamthaminije?
THINK TWICE MY FELLOW WOMAN!!

Bila jina alisema ...

Mumeo hata kama unampenda vipi siku ya kiama atafufuliwa upande mmoja umeoza. Nikuulize swali mtu aliyefufuliwa ubavu mmoja umeoza anaweza kuingia peponi?

Wanaume wameruhusiwa kuoa mke mwingine iwapo tu watakuwa waadilifu. Na imesemwa wazi ndani ya Quran kuwa iwapo hutaweza kuwa muadilifu basi oa mke mmoja. Huyo mumeo hana uadilifu na anafanya upendeleo wa wazi wazi. Sikushauri uondoke kwani wewe mwenyewe mume unampenda. Ila kuwa mvumilifu na mwangalifu, zidisha sala za usiku sana muombe Mwenyezi mungu akuondolee mtihani uliokuwa nao. Sali sala za haja usiku mwingi na ushinde kutwa nzima unafanya uradi kwa kutumia majina ya Allah. Kanunue kitabu cha majina ya 99 ya mwenyezi mungu. Weka CD ya Quran iwe inasoma surratil Baqarah kila siku. Soma ayatul kursiy, soma Iklas 3 kila siku, soma suratil falaq na nasi, kama ulikuwa husali basi sali sasa.

Ukiweza funga siku 7 na kila unapotaka kuanza kufturu muombe Mungu akuondolee mabalaa, fitna, uadui na uhasidi, akupe afya njema na akukinge na kila lililo baya. Usimtaje mtu jina wala usiombe mke mwenzio aachwe maana utaachwa wewe.

Fanya hayo na wala usijishughulishe kutaka kuona wala kujua mke mwenzio kafanya nini wala kapewa nini. Badilika kabisa kazana na ibada, na mume akimsifia huyo mkewe kwako, mwambie nakupa miezi mitatu ukae na bimdogo ufaidi uzuri wake. Akikubali itakuwa imekula kwake kwani wewe utapata muda mzuri wa kufanya ibada zako. Trust me Mungu hachezewi wala hajaribiwi, uje utuletee majibu hapa!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom