Ijumaa, Novemba 25, 2011

FAHAMU MAAJABU YA NANASI KATIKA KUJENGA MWILI WAKO

Katika faida kubwa zinazoelezwa na wataalamu mbalimbali duniani ni uwezo wa tunda hili nanasi katika kutunza ama kuboresha uwezo wa ubongo wa mbele ambao unatumika kutunza 'kumbukumbu' kwa ulaji wa nanasi hadi mwisho wake kila siku kutampa mlaji faida nyingi ikiwemo kusaidia wagonjwa wenye upungufu wa damu unaoweza kujitokeza kwa sababu kadhaa ikiwemo homa za malaria ,typhoid ,minyoo na aina nyingine za magonjwa .
Baridi yabisi ,ukiwa ni ugonjwa ambao sababu za kuibuka kwake unaelezwa kuwa huletwa na ulaji wa nyama ambapo husabadisha kurundikana kwa 'uric acid' katika misuli na viungo vya mwili husababisha maumivu,makali ya viungo na misuli kwa ujumla.
Kwa akina mama wanaonyonyesha na wanaopitia shida ya kutoa maziwa ,wataongeza viwango vya maziwa bila kusahau wale wenye mimba ni vema sana  wakazingatia ulaji wa nanasi.

Vipande viwili ama vitatu vya nanasi au bilauli moja ya juisi ya nanasi ukitumia dakika 15 kabla ya mlo unaweza kutibu matatizo ya tumbo ,bandama, ini ,utumbo mwembamba,vidonda vya mdomoni bila kusahau matatizo ya koo.


NB:Kama utazingatia ulaji wa matunda ya aina mbalimbali kwa wingi tangu msimu wa matunda ya aina fulani utakuwa umejiwekea kinga kwa magonjwa mbalimbali.
          IMEANDALIWA NA ANNETH NYONI

Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

asanteni sana Aneth na Adela nitajaribu ili nione maajabu hayo

Bila jina alisema ...

jamani hii blog inamambo mazuri

Bila jina alisema ...

nimeipenda hii lazima nijaribu nione matokeo yake naitwa Lina

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom