Mimi ni mwanamume naomba ushauri kupitia blog yako Adela katika maisha yangu nilibahatika kuwa na mwanamke ambaye nimezaa naye watoto mapacha wakati nikiwa masomoni kutokana na kwamba nilikuwa nasoma chuo sikuwa na uwezo wa kuwalea wale watoto kwa wakati huo, nilimuachia mzigo mwenzangu,, ambapo baadaye alihama kutoka Dar na kwenda kuishi Mwanza na wazazi wake,,
Baada ya kumaliza chuo nilipata bahati ya kwenda kusoma Uingereza ambapo nimeishi takribani miaka mitano na kwa wakati wote sikuwa na mawasiliano na yule msichana niliyezaa naye sasa hivi majuzi nimerudi nakuanza kumtafuta nilimpata Dar es salaam tena kaolewa na watoto wangu amewapa majina ya huyo mume wake alipowaandikisha shule, na huku wakijua kuwa yule ndiye baba yao mzazi kwa sasa wapo darasa la pili.
nimejaribu kumuambia mama yao nahitaji watoto wanitambue kama baba yao amekataa tena anadiriki kuwaambia watoto wangu kuwa mimi ni mchuna ngozi naua watu naumia sana kwani wale watoto ni damu yangu sijui nifanyeje ili nisiwapoteze.
Baada ya kumaliza chuo nilipata bahati ya kwenda kusoma Uingereza ambapo nimeishi takribani miaka mitano na kwa wakati wote sikuwa na mawasiliano na yule msichana niliyezaa naye sasa hivi majuzi nimerudi nakuanza kumtafuta nilimpata Dar es salaam tena kaolewa na watoto wangu amewapa majina ya huyo mume wake alipowaandikisha shule, na huku wakijua kuwa yule ndiye baba yao mzazi kwa sasa wapo darasa la pili.
nimejaribu kumuambia mama yao nahitaji watoto wanitambue kama baba yao amekataa tena anadiriki kuwaambia watoto wangu kuwa mimi ni mchuna ngozi naua watu naumia sana kwani wale watoto ni damu yangu sijui nifanyeje ili nisiwapoteze.
Maoni 17 :
Tulia tu jamaa yangu, wale watoto ipo siku watatafuta baba yao wa kweli.
yaani kuna siku watapata dharura fulani au tafrani fulani hivi, na hapo ndipo watazinduka na kumwambia mama yao awaambie baba yao au watamwambia tupeleke kwa baba yetu au wenyewe watakuja maadamu sasa wamepata habari kama hizo.
Ulifanya makosa sana bila kuweka utaratibu wowote ukaondoka kwenda uingereza na bila mawasiliano hata matunzo kwa watoto.
Huna maana we mwanaume uligombana na huyo mwanamke na si watoto iweje hata watoto ukawasahau? leo ndo unajifanya unawajua acha ukufanyie hivyo hivyo pumbavu zako kabla hujaenda uingereza ungemtafuta mmalize tofauti zenu ili watoto wa kutambue ukajiona mjanja miaka 5 hujui watoto wanaishije huna akili sasa ndo unatambua dhamani ya watoto? imekula kwako,watu ugombana na kuachana lakini watoto ni lazima uwajali hata kwa kuwajulia hali zao tu inatosha lakini wewe ukajiona mjanja kutowajali watoto wako leo unatambua ni damu yako. loh imeng'ata kwako pole sana,namsifu huyo dada na atakujambisha mpk ukome. Pumbavuuuuuuuuuuuuuu
Me hsia zangu zinantuma kuwa ww ulipompa huyo binti mimba ulimkataa na ndio maana hukuwa na mawasiano nae kwa kipindi chote hicho cha zaidi ya miaka mitano. Kama n kweli hukuwa na uwezo wa kuwatunza hao watoto ulitakiwa kukaa chini na mwenzio na kumwambia ukweli kuwa hv na hv na hv na hv lkn ww inaonekana ulimkataa na ndio maana hataki watoto wakutambue na ameolewa, me nadhani km mngelikuwa na mawasiliano bac acngekukataza kukutambulisha kwa wanao mtakuwa hamkuwa na maelewano kwa kpnd hcho chote. Nani asiejua kuwa aclimia kubwa ya wanaume huwa wanakataa mimba zao na badae kuja kudai watoto!!! NDO MJFUNZE NYIE WENGINE.
Heeeee Hongera sana mdada, hata ingekuwa mimi ningekufanyia hivyo hivyo tena zaidi ya hivyo. yaani wewe hukuwa na pesa, yaani hukuwa hata na muda wa kuenda kuwasalimia na kuonyehs unajali na kuwapenda wanao. ukaondoka kwenda Uingereza, hata viguo tu vya watoto hukuviona huko..leo umerudi baada ya miaka mitano ETI NDO NYOOOOOOO watoto(umebana pua)wangu niwapataje...nakushauri ingia mitini...SEPAAAAAAAAA usitutie kichefuchefu. Tena mimi ndo ningewaambia watoto kuwa ulitaka kuwaua wakiwa wadogo wakuchukie milele...KWENDA ZAKO KULEEEEEE
yaani we mwanaume kl nikifungua hii blog na kukukuta tena unani boreajeeeee.... wadau endeleeni kumpa vidonge vyake mi nshampa hapo juu narudia tena pumbavuuuuuuuuu!!! ingekuwa mm ndo unakuja kwangu kudai ntakutumbuatumbuaaaaa pumbavuuuuuuuuu
Mary
asanteni kwa ushauri mimi ndiye niliyeomba ushauri kweli nilikosea lakini nilikuwa naomba nafasi nyingine niwalee watoto wangu haikuwa dhamira yangu kuwatelekeza kwani kipindi naenda Uingereza mwenzangu tulikuwa hatuna mawasiliano na wakati wote nikiwa huko nilikuwa namuomba Mungu sikumoja tuje kuonana natamani sana kuwa karibu na watoto wangu sijui nawezaje kuomba msamaha ili mama wa watoto wangu anielewe mimi ni binadamu natamani kupata nafasi nyingine niwahudumie watoto wangu
USIJE HARIBU NDOA YA MWENZIO, STAY AWAY!!! ULISHINDWA HATA KUAZIMA SIMU KWA MTU UKATUMA MSG YA KUJULIA WATOTO HALI! AU UNAFIKIRI UBABA NI KUZALISHA TU HALAFU MWANAUME MWENZIO ALEE! AAAGH!!!!, ALIELEA NDO BABA, WEWE HUTAMBULIKI, FUTA AKILINI MWAKO KWAMBA UNAWATOTO
NA ANGEIOA MIMBA KWA SABABU UMEMTELEKEZA, UNGERUDI KUTAFUTA KABULI AU!, PLIZ MUACHE DADA WA WATU NA PIA UNAWACONFUSE WATOTO, MARA BABA LEO HUYU, KESHO YULE, BIG NO!!!!!!!
HATA NINGEKUWA MIMI NISINGEKUPA NA WATOTO WANAJUA YULE NI BABA YAO SO IMEKUL;A KWAKO YANI ANDIKA UMEUMIA NDUGU HAO WATTO HAWEZI KUKUPENDA WEWE TAPELI ULIVYOENDA UK HUKUJUA KAMA UNAWATOTO??ULIVYORUDI NDIO UKAJUA NI WAKO NYOO TENA MIMI NINGEWAAMBIA HAO WATOTO WEWE NI BAKA BAKA WAKAE MBALI NA WEWE SIKU NYINGINE USIRUDIE TENA!! TAPELI MKUBWA WEWE NA UINGEREZA YAKO
du e bwana hiyo imekula kwako haiwezekani huna hela ukakosa hata nafasi ya kwenda kuwaona watoto wako na ingekuwa vizuri kama ungeshirikina na mwenzako katika kipindi hicho kigumu cha kulea mapacha leo hii asingekusaliti. wewe ni mshenzi tena mpumbavuuuuuuuuuuu. tafuta mwanamke mwingine akuzalie watoto ulee na wewe uone ni kwa kiasi gani mwenzio alipata shida na hao watoto tena amapacha. pumbavuuuuuuuuuuuuuuu kabisa we sijui mwanaume gani bwege wewe
jamani binadamu anakosea mnatukana sana huyu kaka lakini mimi naona anastahili kupewa nafasi kwani hata iweje yeye atabaki kuwa baba wa hao watoto jamani mimi naomba usikate tamaa nenda kamuombe msamaha mwenzio kwani hata Mungu anasema samehe mara saba sabini
mdau unaesema apewe nafasi we unamliwaza tu huyo jamaa hiyo imeshakula kwake pamoja na kwamba ameshasamehewa kumbuka hao watoto wameshakuwa wakubwa na wanajua upendo wanaupata wapi kwahyo ameshajiharibia mwenyewe watoto wa siku hizi wanaangalia upendo na ukichanganya na kwamba walishaambiwa historia ya baba yao kamwe hawatakuwa na upendo na baba yao bali ktk kujiliwaza labda ataendelea kuwa baba yao biologically, pole weeeeee
Mary
Mshenzi wewe ulikuvyomuacha alivyokuwa na mimba atena alivyo zaa ukaona ni mapacha ndo ukaamua kwenda UK iliusitoe hela ya matumizi yani ingekuwa ndo mimi huyo dada style ingekuwa hiyohiyo na aseme wewe ni chinjachinja kabisa nyooooo wakikuwa ndo mwawataka wakiwa tumboni mnatoka nduki akiwa staa ndo usiseme nyoooooooooooo
Pole kaka, mtaka mawili lazma moja ukosa. Hapo unakazi kweli kweli.
Mie ushauri wangu kwa vile umefanya kosa kubwa sana, fidia millioni 20 tsh, na kupiga magoti na kutambaa kama mtoto kuelekea kwa mama watoto huku unalia kama mtoto mdogo, na zigo la pesa mkononi unamkabithi. HAPO NAZANI UTASAMEHEWA.
La kufanya, Omba mkubwa wako yeyote yule akusaidie kuitisha mkutano wa kuomba msamaha kwa mzazi mwenzio.
Kikao kiwe cha kifamilly tu, akiwemo mama watoto na mumewe, wazazi wako na wake. majamaa kutoka pande zote mbili, na mashaidi wanao jua kama watoto ni wako.
Siku hiyo inabidi ulie uwezavyo kwa nguvu zako zote na kujiona kabisa kama kipindi kile ulikuwa MPUMBAVU, akili zilikuwa hazija komaa kichwani hila sasa umetubu makosa yako.
Na jua hapo kuna matatu.
Wakukatalie,
Ama wakuambie uwape muda wakafikirie
Ama wakusamehe hapo hapo na wakukubalie watoto ni wako, ila wasikubali ukae nao wewe. INABIDI UKUBALI TU MATOKEO KAKA.
Lakini jua mwisho baada ya mwisho utapata jibu positive, hata kama ikichukua miaka. Kilio chako tu kitawaumiza na watajua kuwa hata wewe ni binadam, na unajua ulikosea na umetubu.
Lakini kwakweli we kaka unakazi kubwa, husifikiri eti utapata hao watoto kiraisi raisi.
Unadeni kubwa. Hata huko UK wanaume upigwa mafain wanapo dai mtoto ambae hawakumudumia, kulipia malezi ya mtoto. Na kama mwanamme hana uwezo basi haki ya mtoto hana, yule alie na uwezo ndio mwenye haki ya kuwa na mtoto.
wewe inabidi ulipie miaka yote tisa ulio watelekeza. 9 mara 2.
Watoto mapacha kulea tabu kweli kweli, mie nimezaa mapacha najua.
ok, nakutakia kila la kheri kaka ufanikiwe. SALMA
Pumbavu, cameroon kabisa, hivi bado u have strength za kuja kutusimulia huu upumbavu.
Nyoooo, ubaba ni kulea babu eeh
so kuweka mimba.
Mvunjifu wa ndoa ya mwanamume mwenzio.
Nawe tafuta mdada mwenye watoto wawili umuoe kisha uwatunze na uwape majina yako.
Nyang'au!
Eeeeh jamani wadau mbona hasira na matusi vimewajaa hivi jamani jamaa kesha sema anaomba second chance bado mnamtukana tu.....DONT YOU BELIEVE IN SECOND CHANCES?
Ni nani kati yenu ambaye hajawahi kukosea na kuamua kujirekebisha then maisha yakaendelea?
Huyo mama hata kama atawaambia hao watoto wasimtambue baba yao atakuwa anawadanganya tu hao watoto.."YOU CAN NOT CHANGE THE HISTORY/PAST.
Kaka nakushauri tumia watu wazima watakusaidia kusema na huyo mama kama wewe hakuelewi, inawezekana anaogopa kuharibu ndoa yake but hao watoto ni wenu...habari ndo hiyo!!!
ww anonymous wa nov, 28 nahisi ni mwanaume kwa mujibu wa comment yako!! ila ukweli kutia mimba cyo kazi wala kupokea mimba ila issue ni kulea mimba hadi mtoto (watoto) hivyo huyo dada anayohaki kufanya hivyo tena nina mpa 100%
mwisho bi dada endelea na msimamo wako huyo anaye kulelea watoto ndio baba wa watoto wako huyu mwingine ni tamaa tu ameona upo kimvulini anataka kukurudisha juani alipokutelekeza hana haja na watoto huyo !! hakutegemea km yupo mwanaume angeliweza kukurudisha kimvulini.
2nza ndoa yako bi dada huyu shetani ucmpe nafasi asilani abadani "Mwanamke Mpumbavu Huvunja Ndoa yake kwa mikono yake"
Sra
du umekuja na gia ya uingereza masomon,kaka hata kama watoto ni wako but stll we n muuaji et nilikuwasina uwezo msom mzima huoni haya kutueleza upumbavu wako,na wanakushauri katafute watu wazima et ukalie kama mtoto wanakudanganya ww n bwege mtunzen na mwoga wa majukum so hata ukipewa watoto hao ukpata chance ya urusi naulimbukeni wa ulaya utawatosa tu na kuwafanya watoto wa mtaan kula kona tapel nyota yako toka asubuh ni uuaji tu
Chapisha Maoni