Ijumaa, Novemba 18, 2011

KANUNI ZA ULAJI BORA

Kitaalam tunaambiwa unachokula leo ndio kinaamua hali ya afya yako kwa siku za usoni ,hivyo basi ni muhimu sana kuzingatia ulaji bora wa chakula na si kula alimradi umekula .katika makala hii tutaangalia kanuni chache na za muhimu katika ulaji bora wa chakula kwanza kabisa inashauriwa kula mara tatu kadri uwezavyo lakini ni afya zaidi kula mara mbili kutwa na pia usile chochote katikati ya milo kwa kuwa ni muhimu sana kwa tumbo kupumzika.

Zaidi ya yote wakati wa jioni hakikisha unakula chakula chepesi .matunda na mboga (green vegetable)visichanganywe kwenye mlo mmoja ila ikibidi sana pitisha muda wa nusu saa hadi saa moja kula tunda ama mboga ya majani unapokula matunda na mboga kwa pamoja unatengeneza sumu iitwayo "uric acid" ambayo huumiza tumbo.

Kula taratibu na tafuna vizuri kwa sababu utaratibu wa kumeng'enya chakula huanzia mdomoni suala la maradhi ama afya lipo mdomoni na sitara yake ipo  katika kusagwa.kamwe usinywe maji huku unakula kunywa kabla ama baada ya mlo vinginevyo kutatokea shida kubwa ya kuchelewa kusagwa kwa chakula.ukizingatia haya unajenga afya bora katika mwili wako.

IMEANDALIWA NA ANETH NYONI

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom