Alhamisi, Novemba 10, 2011

Nampenda sana huyu mwanamke lakini ni mchoyo nifanyeje ili kurekebisha tabia yake.

Mimi ni mwanamume na nimfuatiliaji mzuri wa Blog yako Adela naomba ushauri kupitia blog yako ninaye mchumba nampenda sana tupo katika mahusiano takribani miaka miwili najua ananipenda lakini kuna tabia yake sijaipenda hapendi mimi niwasaidie ndugu zangu kuna wakati mwingine nikimuachia hela na kumuachia maelekezo awape wadogo zangu analalamika na baadaye akija kuwapa anaipunguza na kuwapa kidogo, nilishawahi kumwambia kuhusu tabia yake lakini naona anaendela nayo yaani hata ndugu zake wakiniomba msaada ananiambia nisiwasaidie sasa nashindwa kuelewa kama huyu mwanamke atabadilika au ndiyo tabia yake itabaki kuwa hivyo inanikera sana naombeni ushauri

Maoni 9 :

Bila jina alisema ...

m.ke wa namna hiyo ni mbaya,hatoelewana na ndugu zako kabisa.wakikutembelea,kwa uchoyo wake itajulikana tu,kwa kuwa hujamuoa hali iyo,jee ukiwa nae ndani itakuwa mbaya zaidi.kama hajabadilika hapo mwanzoni,hiyo baadae ndio kabisa hato weza

Bila jina alisema ...

hahaha, hilo ndio tatizo eh?

Mie mtazamo wangu huyo mwanamke naona anawivu wewe kugaia vitu vyako ndugu zako na ndugu zake.

Sababu yeye anaona vyote juu yako, yeye ndio mmiliki na ni vyake yeye peke yake, na ukitoa anaona kama umemsaliti.

Na pengine anaona umewapa ndugu kipaumbele kuliko yeye. Yeye anataka umuweke mbele yeye.

Vile vile kaona ndugu wanataka kukunyonya nguvu zako, na pengine anataka hela zako ujistareheshe wewe mwenyewe na yeye tu basi.

UMEELEWA HAPO KAKA?

Hivi unataka uwasaidie hao ndugu kipesa hadi lini? wao wenyewe hawana akili ya kujua wafanye nini?

Bila jina alisema ...

hahaha, hilo ndio tatizo eh?

Mie mtazamo wangu huyo mwanamke naona anawivu wewe kugaia vitu vyako ndugu zako na ndugu zake.

Sababu yeye anaona vyote juu yako, yeye ndio mmiliki na ni vyake yeye peke yake, na ukitoa anaona kama umemsaliti.

Na pengine anaona umewapa ndugu kipaumbele kuliko yeye. Yeye anataka umuweke mbele yeye.

Vile vile kaona ndugu wanataka kukunyonya nguvu zako, na pengine anataka hela zako ujistareheshe wewe mwenyewe na yeye tu basi.

UMEELEWA HAPO KAKA?

Hivi unataka uwasaidie hao ndugu kipesa hadi lini? wao wenyewe hawana akili ya kujua wafanye nini?

Bila jina alisema ...

Tabia haina dawa,muache tu mapema na uchoyo wake.Kwa familia za kwetu utaacha kuwasaidia ndugu kweli?Huyo siyo chaguo zuri na ushukuru amekuonyesha mapema kabla ya ndoa kwa hiyo "kazi ni kwako"

Bila jina alisema ...

Kama umempenda sana na umemzowea muoe mradi ushamjua tabia yake naamini utajua namna ya kuishi nae /kusaidia wale wanaohitaji msaada kutoka kwako ikibidi utaweza kuwasaidia na bila mkeo kufahamu, mbona wapo wengi twawajua. Cha msingi ni kufahamu kuwa pamoja kwamba atakua ni mkeo lakini kila kitu kina mipaka usiwatupe nduguzo. Na unatakiwa uelewe kwamba unapotoa kwa anayehitaji na akashukuru basi unaongezewa Lakini yategemea na imani yako.

Bila jina alisema ...

wewe kaka dunia hivi sasa ndio ilivyo chenu ni chenu tu ina maana wewe na mkeo au g/friend wako,sio na ndugu zako na wewe unataka ushikwe masikio kama Diamond kwa Wema Sepetu? mpaka mama yake kafikia kuvunja uchumba ? Wasichana wa kileo wanaishi hivyo sio wewe ufikirie mama yako na ndugu zako wakati ninyi wenyewe hamjatatua yenu, AU BROTHER UMEZALIWA USWAHILINI? mpaka uishi nyumba moja na mama yako na mjomba na binamu zako ? kama alivyoshindwa kuishi Diamond bila mama yake? Chagua moja mpenzi wako au ndugu zako na sijui utawajigijigi hao ndugu zako

Simon Kitururu alisema ...

Kwa bahati mbaya watu wengi hawabadiliki kirahisi!:-(

Na kwa bahati mbaya machale yamchezayo mtu mara nyingi ndio ukweli wenyewe.

Na kwa bahati mbaya aulizaye swali kama lako kwa kawaida ana jibu tayari ingawa hataki kuliamini!:-(

Ni mtazamo WANGU tu huu!

Bila jina alisema ...

asanteni sana kwa ushauri jamani mimi ndiye niliyeomba ushauri hii tabia ya huyu mwanamke imenishinda yaani imefika kipindi anaona wivu mimi nilikiwa na marafiki zangu au wakija kunitembelea nikinunua vinywaji anachukia kuna baadhi ya marafiki wananiambia nimuache lakini nikitaka kumuacha analia na kudai kuwa ananipenda

Bila jina alisema ...

Chaguo lako, ni maisha yako. Kuna mengi utakuja kuyaona. Huyo mchoyo, utamuacha. Mwingine next atakuwa anataka kukufanya ATM, na kugawa pesa na vitu bila mpangilio na kukufirisi,utamuacha. Next wa huyo atakuwa mlevi na mzululaji, next wa huyo atakuwa changu doa, na atapendwa na kugawa K hadi kwa marafiki zako na ndugu zako, mwisho utaishi bachelor. Je kuna binadam hasie na kasoro?

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom