Jumatano, Desemba 28, 2011

"Nimemfumania mume wangu akiwa hotelini na mwanamke aliniaga anaenda kusherekea sikukuu Arusha"

Mimi ni mwanamke jamani inaniuma sana kwani nilikuwa nampenda na kumuamini sana mume wangu ambaye tumebahatika kupata watoto wawili,,Sasa hivi majuzi kabla ya sikukuu ya Krismasi mume wangu aliniaga angeenda Arusha amealikwa na rafiki yake kipenzi ambaye hata mimi namfahamu aende Arusha lakini cha ajabu haikuwa hivyo.

 Ilipita kama siku mbili toka aliponiaga rafiki yangu mmoja alinipigia simu na kuniambia amemuona mume wangu Hoteli fulani hapa jijini Dar es salaam sikutaka kuamini ilinibidi niende mwenyewe kuhakikisha jamani nilichokikuta ni kweli alikuwa mume wangu na mwanamke wamekaa kwenye swiming pool wakipunga upepo huku wakiwa wamekumbatiana kimahaba yaani nilitamani kuzimia nilishindwa kufanya chochote ilinibidi nirudi nyumbani huku nikilia kwa uchungu natamani niondoke hapa nyumbani kwani pamoja na kumfumania hajarudi nyumbani hadi leo nilimpigia simu ananiambia atakuja siku yoyote kuna kazi anafanya jamani mimi nifanyeje huyu mwanamume ananipenda kweli niko njia panda natamani kuondoka nyumbani. nisaidieni kwa ushauri

Maoni 15 :

Bila jina alisema ...

Wewe dada uliyefumania mume wako, nina shwali.......Kwanini Mumewe alikwe mahali kwenye sikukuu kama Chrismas bila familia yake?
Pili ulivyomfumani ulienda kumconfront au ulirudi nyumbanikimya bila yeye kujua?
Unaonesha uthaifu wako kama Mke wa ndoa hukuchukulia issue kama mwanamke mjasiri, kwanza Mumeo kitendo cha kukuaga anaenda Arusha bila wewe, anaonekana ni jinsi gani anajua uthaifu wako. Grow up dada.....Pole, ndoa si lele mama

Bila jina alisema ...

UNAONEKNA ULINGANGANIZA HIYO NDOA EITHER ALIKUOA KWA KUWA ULISHAPATA MIMBA MWANAUME AKIFUMANIWA LAZIMA ANGERUDI KUKUANGUKIA

PENZI ALILAZIMISHWI WANAWAKE TUMEZIDI!

Bila jina alisema ...

hivi wewe ni mke wake au kimada wake? Inawezekaneje mumeo aalikwe na rafiki yenu peke yake badala ya kwamba mlialikwa wote muende Arusha.Haiji akilini mimi mume wako nikuache eti naenda kula xmas peke yangu bila wewe na watoto wetu. Au kulikuwa na sababu muhimu ya yeye kwenda peke yake, lakini iweje awaache familia siku kama hiyo peke yenu?

Hii hadithi kama ya kutunga tu haileti maana yoyote, kwamba kweli umkute mumeo katika mazingira hayo na bado akae hukohuko, na wala hujasema ulipowakuta lifanya nini na yeye mumeo alifanya nini?

Kama kweli hilo lilijiri basi muhimu mvumilie tu na zungumzeni yaishe maana hukuwakuta wanafanya kitu chochote.Unachoweza kukomalia hapo ni ule udanganyifu wa kwamba anaenda Arusha na kumbe bado yupo Dar.

Bila jina alisema ...

kuondoka nyumbani siyo solution.umeshafikiria kuhusu watoto wako wataishije baada ya kuondoka hapo?najua inauma bt u hv to thing about ur self and ur children coz any wrong decision u make will affect them.huyo mumeo inawezekena isiwe akili yake so you have to stand by him and your family.

Bila jina alisema ...

asanteni kwa ushauri wadau mimi ni mwaanamke niliyeomba ushauri wakati mume wangu ananiambia anaenda kusherekea sikukuu mimi nina mtoto mdogo kwasasa nilijifungua kwa operation kwahiyo sikuweza kumlazimisha tuende wote hivyo nilimuambia tu aendena mimi sikuwahi kufikiria kama alikuwa na nia tofauti ndiyo baadaye yote hayo yakatokea juzi alikuja nyumbani hakuongea chochote alichukua baadhi ya nguo na kuondoka nimemuuliza anasema kuna kazi anafanya na alikuwa hataki maswali zaidi nipo katika wakati mgumu jamani kwani simuelewi hata kidogo huyu mwanaume amebadilika sana

Bila jina alisema ...

NDO WALIVYO HAO KAMA UNAWEZA JITAHIDI KULITOA TARATIBU KWENYE MOYO WAKO UTAWEZA TU MAMII THEN KAMA UNAPIGA KAZI KAZANA KWENYE KAZI YAKO JIPANGE KIVYAKO HATA AKIHAMIA HUKO NYUMBA NDOGO HUTETAREKI HUWA NI WASHENZI SANA HAO NA USIKUTE KALONGWA HAPO ALIPO CHEZEA WADADA WANATAKA KULA KUVAA NA KUJENGEWA KUPITIA MUME WA MWENZIE.SO TAKE CARE DEAR.POLE EEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEH.

Bila jina alisema ...

Masikini pole mwanamke mwenzangu, hapo kuna 2, la kwanza kama unafanya kazi angalia maisha yako na watoto wako achana naye na la pili kama ndiye unayemtegemea vumilia mtoto akue huku unachakarika kutafuta kazi au biashara kimya kimya usimuoneshe kisirani wala nini ila kwenye tendo la ndoa hakikisha unatumia kinga ndugu yangu.

Nakwambia hivyo sbb muda wa kunyanyaswa na hao viumbe umekwisha na huyo mume wako anaonesha wazi wazi hakupendi km ulivyo coz asingefanya hayo anayoyafanya ukizingatia ww uko kwenye uzazi tena operation, shm on him, imeniumiza sana kwa kweli.

Na ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo angalia ni wp unakosea la km ni kawaida yake km utapenda ushauri wangu fuata na pia washirikishe wasimamizi wa ndoa yenu ht wazazi japo ni aibu bt hakuna jinsi coz always mama ndiye mlezi unatakiwa usimamie future ya watoto wako wababa wanajua kujaza mimba tu.

Na kingine pendelea kufungua website zinazohusu mahusiano kuna mafundisho mengi tu kuhusu maisha ya ndoa sio yote tunapewa kwenye kparty.

Pole ndugu yangu.

Bila jina alisema ...

wakati umekwenda kufumania alikuona au hakukuona na huyo kimada alikuona pia.mimi ushauri wangu kwako kaa hapo nyumbani kwako hakuna kuondoka kwenda popote na wala huna haja ya kumuuliza mumeo unamuuliza nini na wakati umeshaona uliyotaka kuyaona.kama unaipenda hiyo ndoa hakuna kuondoka wanakwendaga huko mwisho wa siku wanarudi haoo hawana maana.lea mwanao bibi wee achana nae kabisa.

Bila jina alisema ...

Awali ya yote pole kwa huo mkasa, naamini ni masa wa kweli sio wa kutunga kama ambavyo mzungumzaji aliyepita ameutilia shaka kwani maelezo yako yalikuwa pungufu fulani hivi ambayo msomaji makini kama huyo ama mwingine yeyote angeweza kuutilia shaka.

Turudi kwenye mkasa wako.
Sikushauri uiache familia ama muachane na huyo bwana HAPANA ila kwanza jaribu kujiridhisha ikiwa na maana chunguza kwanza chanzo cha tatizo usikimbilie kutaka kuachana.
Pili naungana mkono na aliyesema historia yake ikoje huyo bwana je amekuwa na matendo ya kutia shaka, umeshawahi kufuma sms yoyote tatanishi kwenye simu yake na mambo mengine mengi alimradi yawe ya kukusaidia katika uchunguzi wako, ama ndio mara ya kwanza, wewe unamjua vema mumeo kuliko sisi tunaoandika.

Baada ya kukamilisha uchunguzi wako mkalishe chini mzungumze ninyi wawili kwanza kabla hamjalitoa nje kwa watu wengine, halafu hebu muulize kama wewe ukifanya hivyo siku moja atafurahi, wala usizungumze nae kwa kupanic jipange tu, wanawake mmepewa ushawishi na Mungu tumia kipaji hicho, kama anakuwa mjeuri na hataki kukaa na kuzungumza ili muyamalize kwa amani ninyi wawili basi ita wazazi wala asikutishe wala kukunyanyasa,naamini mtafikia muafaka dada.

kumbuka wanawake wa mujini siku hizi wana mambo yawezekana kashawekwa sawa anaona upande mmoja tu wa shilingi haoni wa pili tena, mambo hayo yapo ila simaanishi kuwa mumueo kawekwa sawa ila ni mambo ambayo yapo, hasa kama ana kipato kizuri.
Natamani kuendelea kuandika ila nisikuchoshe kwa maneno mengi.
Mike.

Bila jina alisema ...

Pole bibie.

Mimi mwanaume nimekuhurumia sana.Nimefikiri kama ndo ningemtendea mke wangu ambaye tumezaa watoto 5 wazuri halafu niondoke kwenda kula Xmas nikuache unahangaika na watoto huku nimekudanganya du!! Yaani huo mwiba.

Nakusihi sana kaa hapo home angalai watoto, na inawezekana kama kweli ulimfumania, basi yamemfika shingoni anashindwa kutema na kuomba msamaha amejaa aibu ndo maana amekaa kando kidogo ili angalau yavinde.Usiondoke bibie atarudi tu.

Ila hujatuambia ulipomfumania ulifanya nini?na je alikuona pamoja na huyo aliyekuwa naye?

Je, vipi mna ushirikiano mzuri katika mapenzi?

Bila jina alisema ...

Pole sana mwanamke mwenzangu naelewa unavyojisikia kwani hata mimi yalishanikuta kama hayo tena nikiwa nimeshazaa watoto wanne, nililia sana na kulaani lakini haikusaidia kwani tabia haina dawa huyo mwanamke sio wa jana wala leo wala wa sikukuu huyo ni wa siku nyingi. Nilishirikisha wazazi na ndugu wote walinishauri nikae watoto wakue huku natafuta kazi, niliishi kwa kinyongo lakini sikumwonyesha zaidi ya kujipanga kimaisha. hatua ya kwanza ilikuwa kumtoa moyoni kabisa ingawaje ni ngumu kwani nilikuwa namwona, pili hakuna kutaka ngono hata alikuwa akinihitaji ilikuwa ili mradi hakuna bashasha wivu ukamvaa, tatu nilitafuta chuo na kujiunga hivi sasa nafanya digrii ya pili, amenyooka ile mbaya ukizingatia niliolewa nikiwa nimemaliza kidato cha sita miaka mingi iliyopita, bc kila mara huko wapi nikikanyaga anakanyaga ana hisi nitasepa hivyo napenda kukutia moyo sana usilie kwa ajili ya mapenzi utakonda, utachuja na hata kama kuna mshikaji pembeni ataogopa kukunyemelea. kula raha , lea watoto, jipende sana kimwili na kiakili na hata mimi nimewapata watoto kwa kisu

Bila jina alisema ...

Pole dada ! Lakini issue yako ni cha mtoto, Umemfumania mme wako na mwanamke na wapo mahala pazuri wanakunywa na kustarehe ? Je mimi niliyemkuta mume wangu na house girl tena kitandani kwangu. Lakini mpaka leo niko naye tunakula raha kama kawaida. Aliniomba msamaha na yakaisha. Wanaume ndivyo walivyo duniani kote toka North Pole mpaka South Pole, hata mama na bibi zetu walikuwa wanawafumania waume zao huko vijijini lakini walivumilia tu, kwa hiyo asikupe shida jipange, jiweke smart na kujiamini atarudi tu na mtaendelea na maisha kama kawa.

Mama Melvin alisema ...

Pole sana mdada, hawa wanaume wana mambo mengi sana lakini wewe usikimbilie kuondoka nyumbani kwako yeye ndio aondoke kama anataka na atakaporudi usimchekee hata kidogo lazima ajue alichokufanyia sio kitu kizuri tena kasirika sana. Akiamua kukuomba msamaha sio tu umkubalie aahidi kwamba hatakuumiza tena, ukimchekea tu atarudia tena huyo.

Bila jina alisema ...

Pole mwanamke mwenzangu, ila muombe Mungu akupe ujasiri uwalee watoto wako na usikimbilie kuondoka, kama unafanyakazi kaza buti kwenye kazi yako na ujipende kwa kwenda mbele. atarudi tu huyo wanaume ni watu wa ajabu sana.

Bila jina alisema ...

Dada ulichokosea nikutomkabili palepale. Dunia ya leo sio ya bibi zetu kuna UKIMWI. Mwambie ulichoona, usikubali kushirikiana naye kabla ya kupima kama hajali ondoka utateseka mwanzoni baadae utasimama. Ukijing'gang'aniza atakuletea UKIMWI hao watoto watakosa baba na mama, bora wamkose mmoja, baba. Kama hajirekebishi chapa lapa

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom