Jumanne, Januari 24, 2012

Eti wanaume wanaushirikiano kuliko wanawake ???

Vijana wa Passion FM  RADIO 95.8 Dar es Salaam kutoka kushoto Anuary Sanga, Ben Mwanantala pamoja na Dj George niliwakuta wameanzisha hiyo mada kuwa wanaume wanaushirikiano kuliko wanawake .


Anuary yeye alisema "wanawake hawapendani kwasababu ya wivu uliopitiliza ndiyo maana unakuta wanagombana na kusutana mara kwa mara huku akisema haitokei kukuta wanaume wakisutana".

Malyango Mugeta pichani yeye alisema "wanaume wanaushirikiano sana ndiyo maana wanapata maendeleo kwa wingi kuliko wanawake".

Hapa Anuary alikuwa anasema "mfano mimi na Dj George tunaweza kupanga dili la maana na kufuatilia hadi kufanikisha bila ya kugombana lakini madili ya wanawake kwa wanawake maranyingi huwa wanagombana , kununiana, yaani tafrani tupu alisema Anuary

Hapa Ben alikuwa anasema "lakini mshikaji sikuhizi kuna wanawake wana ushirikiano wana vikundi vinawasaidia sana mi naona ni msimamo tu kwani sasa hivi sasa wanawake wanakuja kwa kasi sana katika maendeleo"

"Wanawake wanayonafasi nzuri sana katika maendeleo  muhimu ni kusaidiana na kupendana sasa unakuta mwanamke anakumbia mimi napenda kufanya kazi na wanaume siwapendi wanawake ni majungu tu sasa hapo kunaushirikiano mi nawashauri wapendane".


Ben Mwanantala alimalizia kwa kusema wanawake wanaweza wakishirikiana na kupendana kwa nia ya kujikomboa kimaendeleo.JE WEWE MDAU UNASEMAJE KUHUSIANA NA MADA HII.................................

Maoni 7 :

Edgar alisema ...

Adella, Ingawa wanaume huwa wanashirikiana zaidi kuliko wanawake, sidhani kama wanaume wana moyo wa ushirikiano kuliko wanawake. Nilichogundua ni kwamba wanaume wanaweza kuweka hisia zao(emotions) pembeni kirahisi kuliko wanawake kama wanaona ushirikiano utawaletea manufaa. Kinadada wakati mwingine, huwa wanaruhusu emotions ziwatawale na kuzifuata hata kama maamuzi tofauti yangewafaidisha zaidi.

Edgar alisema ...

Hata wanaume wana wivu, chuki na hizia zote ambazo wanawake wanazo. Tofauti tu ni kwamba mwanaume atauweka wivu au hata chuki zake pembeni kushirikiana na mtu asiyempenda kama anahisi atafaidika na ushirikiano huo. Lakini sista hapo atakwambia "Hell NO!" I'm not working with her... I hate that b*tch!

lulu ibrahim alisema ...

hallow dada mimi nimpenzi sana wa hii blog yako napenda na inanifundisha mengi sana kwenye swala la mahusiano

mimi nakubali tena sana kwamba wanaume wanaushirikiano sana kuliko sisi wanawake kwanza hatupendani

ADELA KAVISHE alisema ...

asante sana lulu na Edgar tuko pamoja sana ila jamani ili suala linategemeana na tabia ya mtu na mimi nahisi ni pande zote mbili mwanamume na mwanamke kuna wanawake wanaushirikano na pia wapo wanaume hawana ushirikiano na sikuzote unaambiwa umoja ni nguvu utngano ni udhaifu

Bila jina alisema ...

mmmh wanawake wana majungu na umbeya yaani hatupendani

Bila jina alisema ...

ASILIMIA KUBWA YA WANAUME NI WANAFIKI SANA NDO MANA UNAKUTA WANAJIFANYA WANAUSHIRIKIANO LAKINI MIOYO YAO IMEPINDA ILA MWANAMKE MARA NYINGI KAMA HAKUPENDI ATAKUONYESHA SANA TU KWAMBA MIMI NA WEWE HAPANA SO HATUWEZI PIGA KAZI PAMOJA ....ILA NOWDAYS KUNA MA DADAZ WANASHIRIKIANO USIPIME HAYO YANAYOENDELEZA CHUKI UJUE NJAA NAZO ZINACHANGIA KWA NJIA NYINGINE MFNO UNAKUTA LABDA SHOST KABAHATIKA KUPATA JAMAA MWENYE HELA ZAKE NA ANAMTUNZA HATARI SO UNAKUTA MWENZANGU NAMIE UNAPATA MISAPATA NDO HIVYO CHUKI INAANZIA HAPO MAANA KILA MTU ANAWISH AFANIKIWE YEYE NDO HIVYO UTASEMWA ANAJICKIA MARA OH ANANATA.COMMY

Edgar alisema ...

Ni kweli Adela inategemeana na mtu. Lakini zidhani kama wanaangalia mtu na mtu, bali wanaangalia kiujumla. Mfano. Wanaweza kusema "wanaume huwa wanakuwaga warefu zaidi kuliko wanawake." Ni kweli.. Lakini ukiangalia mtu na mtu, kuna baadhi ya wanawake ni warefu kuliko baadhi ya wanaume

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom