Jumatatu, Januari 23, 2012

Ulaji wa baadhi ya vyakula wakati mwingine husaidia katika kuboresha muonekano wa ngozi yako

Mbogamboga kama kabichi, brokoli, cauliflower nk. aina hizi za mboga zina kompaundi inayoitwa ' glucosinolates' na 'enzaim' inayoitwa 'myrosinase' kwa kula mboga hizi mbali na kuongeza mvuto katika ngozi yako itasaidia kuikinga ngozi yako dhidi ya kansa.
Vyakula kama karanga, korosho nk husaidia sana kuikinga ngozi yako na mionzi ya jua pia upunguza ukavu katika ngozi

Parachichi tunda hili lina virutubisho muhimu sana katika utengenezaji wa damu hivyo ikiwa utakula mara kwa mara itakusaidia katika utengenezaji wa seli hizo muhimu mwilini

kunywa maji husaidia kunyevusha ngozi na kuonyesha uhalisia wake pia humfanya mhusika aonekane mwenye ngozi changa zaidi ya umri wake, ikiwa wewe ni mmoja kati ya wale wanaopoteza pesa nyingi katika kununua losheni na krimu  kwa nia ya kuboresha muonekano wa ngozi yako waweza kuokoa fedha zako kwa kutumia maji kwa afya hivyo unashauriwa kunywa angalau gilasi nane za maji kwa siku haitachukua muda mrefu kuona matokeo yake kwani hii ni njia rahisi sana pendelea kunywa maji mengi kuliko vilevi, soda ama juisi katika kukata kiu.

bila ya kusahau matunda ya aina mbalimbali

Hii ni siri pekee hata mimi binafsi naitumia katika kuboresha muonekano wa ngozi yangu kuwa ya asili wakati wote
Tunda hili lina virutubisho muhimu vinavyofahamika kama beta-carotene kwa mujibu wa wataalamu wa afya na urembo husaidia sana kupambana na sumu mbalimbali zinazosababishwa na baadhi ya vyakula mwilini.ZINGATIA NA UTAONA MABADILIKO  

Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

Adela hongera sana kwa kuwa na blog nzuri ya kuelimisha nakupenda sana naitwa mama Elly

Bila jina alisema ...

asante sana kwa ushauri na mimi nitaufanyia kazi my dear

Bila jina alisema ...

yaani hii blog naikubali sana inaelimisha ni balaa we mdada nakukubali asante kwa hili

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom