Jumatatu, Januari 16, 2012

Inawezekana mwanamke akampelekea mwanamume kuwa muongo katika uhusiano

Kuna vitu mbalimbali ambavyo wanawake huwa hatupendi kuambiwa ukweli kwa mfano,, unaweza kumkuta mwanamke amevaa nguo vizuri na kujitizama kwenye kioo akaona amependeza lakini atarudi na kumuuliza mpenzi wake mbona hunisifii kama nimependeza?? ikitokea mwanamume akimuambia hajapendeza kwa mtazamo wake basi atanuna kitendo ambacho kitampelekea huyo mwanamume kushindwa kumkosoa wakati mwingine,  atakua anakuambia umependeza wakati haujapendeza ni vizuri kukubali ukweli,, mbali na mavazi kuna mapishi, mwanamume anaweza kukusifia chakula alichopika mwenza wake ni kizuri hata kama ni kibaya alimradi tu amfurahishe mpenzi wake katika hili kuna namna ya kumueleza kwa lugha nzuri ili aweze kujifunza kupika sasa ukimsifia kuwa anajua wakati hajui atajifunza lini.

Ni vyema kwa mwanamke kutambua nini ambacho anakosea ili aweze kutafuta utatuzi na si  kumwambia kuwa yeye ni bora wakati hakuna kitu mfundishe yale anayokosea  na mwanamke inapotokea mpenzi wako anakukosoa basi usilalamike na kuona kuwa hakupendi kaa chini na tafakari ili ujue kipi kilicho sahihi MAPENZI YANAHITAJI USHIRIKIANO PANDE ZOTE MBILI,,Lakini pia kuna ile hali mwanamume ametoka safari au amechelewa kurudi nyumbani unaanza kumuuliza umetoka wapi? akikujibu kuwa ametoka kazini au safari unaanza kulalamika na kusema ni uongo bila kuwa na uhakika na ndiyo maana unakuta wanaume wanasema wanawake hatupendi kuambiwa ukweli. sijui unalionaje hili mdau ni mtazamo tu.......................

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

Ndio inawezekana kabisa lakini inategemeana na msimamo wa mwanaume wengi sana wanakuwa waongo kupita wapenzi wao bila wao kujua Most of them wanafikiria wanawasaidia wapenzi wao kumbe wanajiharibu wao.Kuwa my girl kaniambia nifanye hivi i will do it for her even if it means to lie only this once some of them call it true love kwasababu ameweza kufanya vile mpenzi wake anataka. Sasa utadanya leo na kesho atataka tena mwisho wa siku unajikuta your a great liar.

emuthree alisema ...

Tupo pamoja

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom