Jumatano, Januari 04, 2012

Naitwa Zuhura" Jamani huyu mwanamume ananiaibisha mambo yetu ya chumbani anawasimulia marafiki zake"

Mambo vipi Adela mimi ni mfuatilia sana wa Blog yako naomba uniwekee ujumbe huu nipate ushauri, jamani mimi ninaye mchumba nampenda sana na tumekuwa katika mahusiano takribani mwaka mmoja na nusu lakini tatizo mwenzangu sijui anatabia gani kwani mambo yangu yote anayoyajua anawaambia marafiki zake kuna kipindi niliwahi kumuambia kuhusu tabia yake lakini imekuwa vigumu kubadilika kwani hivi majuzi nilikutana na rafiki yake mmoja maneno aliyoniambia kiukweli nilishangaa eti aliniambia "shemeji mambo yako makubwa anatuambia tu bwana ako kwamba umekamilika kila idara yaani akanitajia hadi nguo ya ndani nayopenda kuvaa na mambo mengine ya aibu yaani nilihisi kama nimevuliwa nguo hii tabia inanikera sana yaani marafiki zake wengine wanadiriki kuniambia shemeji  wewe kwa viduku kitandani tunasikia unaweza sana  sasa jamani huyu mwanamume nimfanyeje kwasababu yamenifika kooni natamani hata kumuaibisha inaniuma sana sikutegemea kama yupo hivyo.

Maoni 7 :

Bila jina alisema ...

khaaa huyo mwanamume inabidi avalishwe gauni achana naye shost mapemaaa hata kama unampenda vipi

Bila jina alisema ...

jamani ana tabia za ajabu sana achana naye vinginevyo uwe na namna ya kumbadilisha hiyo tabia

Mama Melvin alisema ...

eeeeh! sasa ndio mambo gani tena hayo jamani! wewe muonyeshe umekasirika sana kuhusu hilo na uwe muwazi kwake mwambie tu kwamba kama hutaacha hiyo tabia yako mimi na wewe basi. haya ni mambo ya kitoto kabisa.

Bila jina alisema ...

Huyo ndo mwanaume mzuri sana na anakupenda kama anaweza kukusifia hata kwa wenzake huyo ndo mwanaume.

Hao wanaume rafiki zake wanaokuja kukuambia hao ndo haziwatoshi kabisa na wako kukuvunjia mahusiano yenu.Usitoke hapo kama wengine walivyosema kwani mengi yanaweza kuwa ya uongo maana mwanaume mzima ambaye rafikiyo amekupa siri za mpenzi wake zilizo nzuri unazitunza huwezi kwenda mwambia mhusika.

Kuna wengine wanatamani kupata mwanaume kama huyo ambaye ameridhika na idara zako zote.Kwani ulitaka vipi akutukane?Badala ya kufurahi kuwa kumbe unafaa wewe unaghadhibika vipi?Sula muhimu hapo ni kuongea na mpenzio ili asimwage unga penye kuku wengi kwa ajili ya kutunza heshima yenu.lakini huyo ndo mume hasaaaaaa.mfundishe tu jinsi ya kutunza siri na ikiwezekana umwambie kuwa rafiki yake fulani amekuambia kuwa ulimwambia/unawaambia siri za ndani.Hapo atakoma hatarudia tena.Mpe hasara za kutoa siri za ndani ya mahusiano.

Bila jina alisema ...

Mkataze hiyo tabia haifai labnda kama anakunadi kwa hao rafiki zake na asije shangaa mmoja wao akataka kuthibitisha anyohadithiwa

Bila jina alisema ...

wewe binti hao rafikizake wanakuwa wanasimulia mambo yao kwa maana hata wao wanamsimulia yakwao na rafikizao wa kike sasa hao wanataka uchukie uwape wao halafu muachane ingawa na yeye anazidi kusimulia kila kitu

Arusha Computers! alisema ...

Pole sana ila ukweli nikwamba huyo mchumba wako nadhani bado haja kamilika labda na wwe utuweke wazi kidogo kwa upande wa umri wenu maana kama sio mgonjwa basi atakuwa hana malengo na wwe bali kukutumia tu na kukuaniaka kwa wenzake. Chakufanya muite tena na mzungumze katika hali ya kawaida na sio kulumbana den ukiona bado anaendelea ndio tiketi ya kuambiwa kwaheri usisubir mpaka akutamkie tafuta mwingine anae weza kufunga mdomo na sio huyo redio ya kichina.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom