Ijumaa, Januari 13, 2012

"Anataka niache chuo ili anioe, anasema baadhi ya wanawake waliosoma sana wanadharau "

Mimi  ni mwanamke ninaye mchumba tumekuwa wapenzi kwa muda sasa nampenda sana na malengo yetu ilikuwa ni kuja kuoana yeye ni mfanyabiashara elimu yake ni kidato cha nne baada ya hapo hakuendelea na masomo tatizo linakuja anataka mimi niache chuo ili anioe hataki niendelee na masomo nilimuuliza kwanini hapendi mimi niendelee na masomo alisema hapendi kuwa na mwanamke mwenye elimu kubwa kumzidi yeye huku akinisisistiza kuwa inabidi niache chuo nijishughulishe na biashara mimi nampenda sana na pia napenda sana kusoma sasa sijui nifanyeje ili niweze kumfanya mpenzi wangu anielewe na kuniacha niendelee na  masomo yangu naombeni ushauri wenu

Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

wewe kasome akikuacha utampata msomi mwenzio kasome kwanza

Bila jina alisema ...

achana naye huyo akutakii mema

Bila jina alisema ...

Huyo lazima atakuwa mwendawazimu khaaa ana roho mbaya sana kusoma wajibu mueleweshe asilete ushamba

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom