Mimi ni mwanamke ninaye mchumba tumekuwa wapenzi kwa muda sasa nampenda sana na malengo yetu ilikuwa ni kuja kuoana yeye ni mfanyabiashara elimu yake ni kidato cha nne baada ya hapo hakuendelea na masomo tatizo linakuja anataka mimi niache chuo ili anioe hataki niendelee na masomo nilimuuliza kwanini hapendi mimi niendelee na masomo alisema hapendi kuwa na mwanamke mwenye elimu kubwa kumzidi yeye huku akinisisistiza kuwa inabidi niache chuo nijishughulishe na biashara mimi nampenda sana na pia napenda sana kusoma sasa sijui nifanyeje ili niweze kumfanya mpenzi wangu anielewe na kuniacha niendelee na masomo yangu naombeni ushauri wenu
Maoni 3 :
wewe kasome akikuacha utampata msomi mwenzio kasome kwanza
achana naye huyo akutakii mema
Huyo lazima atakuwa mwendawazimu khaaa ana roho mbaya sana kusoma wajibu mueleweshe asilete ushamba
Chapisha Maoni