Ni vigumu sana kuishi kwa furaha na mpenzi ambaye moyoni mwako hauna hisia juu yake. Na hii ni kutokana na kujikuta umependa kwasababu ya maslahi kwamba unachokitaka ni pesa ama umeamua kuishi naye kutokana na kumuonea huruma, vilevile kutokana na shinikizo la ndugu nk, ni jambo la muhimu sana kuzingatia hisia ulizonazo inapendeza na ni furaha kuwa na mwenza unayempenda kwa kila kitu yaani hisia zako juu yake ni za kweli na yeye pia awe na hisia za kweli juu yako vinginevyo kama hakuna hisia za kweli basi migogoro inaweza kujitokeza mara kwa mara na kupelekea kutokuwa na penzi la kudumu furaha yako italetwa na namna ambavyo unafuata hisia zako na si kufanya kwa kuiga, tamaa au kujilazimisha |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni