Katika maisha ni jambo la muhimu kuwa na tabia ya kumfariji mwenzio ikiwa anamatatizo ama amekata tamaa katika jambo fulani mfano katika maisha ya mahusiano ya kimapenzi ni wazi kabisa kila mmoja atapenda apate faraja kutoka kwa mwenza wake lakini siyo inatokea umepata matatizo labda katika sehemu unayofanya kazi ukirudi nyumbani mwenza wako badala ya kukufariji usikate tamaa ndiyo kwanza anakusimanga na kukuzodoa,, Faraja inasaidia katika kumliwaza mtu aliyekata tamaa bila kujua nini hatima ya maisha yake. kwani katika matatizo mtu akikosa faraja inaweza kumpelekea hata kujichukia, kushindwwa kusonga mbele , na hata kujiua. |
Maoni 1 :
Mapenzi yanahitaji ukaribu sana baina ya wapendanao, hata kama mko mbali mbali basi tumieni fursa ya utandawazi ili kujiweka karibu sababu kiukweli mapenzi ya mbali ni hatari no matter what, kama hamuwasiliani hilo halina ubishi..... Ninakiri faraja ndio sababu ya kuwa wapenda nao.
Chapisha Maoni