Alhamisi, Februari 23, 2012

Jamani wivu ukizidi??? Amgonga mkewe kwa gari kisa?? wivu wa kimapenzi

Katika mapenzi wivu unahusika kwa asilimia kubwa lakini ukizidi unaweza kuwa matatizo,, kuna tukio limetokea huko mkoani Mara wilayani Bunda  Mfanyabiashara mmoja anadaiwa kumgonga kwa gari mkewe na kumjeruhi kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.

 Kamanda wa Polisi mkoani Mara Robert Boaz amesema mwanamke huyo anayeitwa Nasra Mohamed mkazi wa mjini Bunda   alipatwa na mkasa huo ambapo siku ya tukio mwanamume huyo aliyekuwa anaendesha gari yake aina ya Nissan T 400 BBC, alimkuta mke wake akiwa anatembea katika barabara kuu ya Mwanza , Musoma mjini Bunda, Imeelezwa kuwa alipomuona mkewe alisimamisha gari lake na kisha akamuita lakini alipomsogelea aliendesha gari kwa kasi na kumgonga na kuanza kuuburuza mwili wake umbali wa zaidi ya mita 150.

 Baadhi ya mashuhuda walidai kuwa licha ya mwanamume huyo kumgonga mkewe hakusimama na kwamba alilitelekeza gari lake katika kijiji jirani baada ya kupasuka gurudumu moja la mbele.Aidha imedaiwa kuwa mwanaume huyo amekuwa akimtuhumu mke wake kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine mjini hapo. Polisi wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanamsaka mtuhumiwa huyo ili sheria ichukue mkondo wake.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom