Alhamisi, Februari 02, 2012

Je unadhani njia gani unaipenda zaidi katika mawasiliano kupiga simu ama kutuma ujumbe wa maandishi??

Kwa asilimia nyingi watu wengi katika kuwasiliana hupenda kutuma ujumbe kwa kupitia simu  kutokana na gharama, lakini pia asilimia kubwa ya watu hupenda kupiga simu,,,,,Aneth Nyoni pichani yeye anasema anapenda kupiga simu kuliko kutuma ujumbe mfupi wa maandishi "napenda kupiga simu kwasababu ni mvivu sana kuandika ujumbe lakini wakati mwingine inabidi niandike ujumbe kutokana na simu inakuwa haina hela ya kutosha" amesema Aneth.

 Binafsi naona ni vyema kutumia njia zote mbili kwani kuna wakati mwingine mtu ukimpigia simu kwa nia ya kumuambia jambo fulani lakini ukashindwa kuelezea vizuri kama ambavyo ukiandika ujumbe hata na hivyo kuna baadhi ya watu ni wavivu kujibu ujumbe sasa unalazimika kumpigia simu JE WEWE MDAU NJIA GANI UNAIPENDA ZAIDI .............

Maoni 5 :

Bila jina alisema ...

yaani hata mimi ni mvivu sana kujibu message yaani bora kupiga simu kama unayo hela

Bila jina alisema ...

hahahaha Adela nimeipendaje hii marafiki zangu huwa wananilalamikia sana sijibu message zao lol mimi napenda sana kupiga unaambiwa tumia hela ikuzoee

Bila jina alisema ...

Npenda kupiga Adela WANGU.WEWE JE?

ney alisema ...

napenda meseji kupita maelezo....yan mtu anaweza piga simu nisipokeee

ney alisema ...

napenda meseji kupita maelezo....yan mtu anaweza piga simu nisipokeee

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom