Kwa asilimia nyingi watu wengi katika kuwasiliana hupenda kutuma ujumbe kwa kupitia simu kutokana na gharama, lakini pia asilimia kubwa ya watu hupenda kupiga simu,,,,,Aneth Nyoni pichani yeye anasema anapenda kupiga simu kuliko kutuma ujumbe mfupi wa maandishi "napenda kupiga simu kwasababu ni mvivu sana kuandika ujumbe lakini wakati mwingine inabidi niandike ujumbe kutokana na simu inakuwa haina hela ya kutosha" amesema Aneth.
Binafsi naona ni vyema kutumia njia zote mbili kwani kuna wakati mwingine mtu ukimpigia simu kwa nia ya kumuambia jambo fulani lakini ukashindwa kuelezea vizuri kama ambavyo ukiandika ujumbe hata na hivyo kuna baadhi ya watu ni wavivu kujibu ujumbe sasa unalazimika kumpigia simu JE WEWE MDAU NJIA GANI UNAIPENDA ZAIDI ............. |
Maoni 5 :
yaani hata mimi ni mvivu sana kujibu message yaani bora kupiga simu kama unayo hela
hahahaha Adela nimeipendaje hii marafiki zangu huwa wananilalamikia sana sijibu message zao lol mimi napenda sana kupiga unaambiwa tumia hela ikuzoee
Npenda kupiga Adela WANGU.WEWE JE?
napenda meseji kupita maelezo....yan mtu anaweza piga simu nisipokeee
napenda meseji kupita maelezo....yan mtu anaweza piga simu nisipokeee
Chapisha Maoni