Jumatano, Februari 08, 2012

Je unafahamu dharau ya mambo madogo inaweza kuleta shida katika maisha????

Katika maisha yetu ya kila siku tunakutana na mambo mengi ikiwemo mazuri na  mabaya,sasa katika hayo mambo  ni muhimu kuwa makini ili usijikute unadharau yaliyo muhimu  mfano kama kudharau kazi ambayo inakuingizia kipato au kudharau kazi za watu wengine,,pia kutoa majibu yasiyopendeza, kutosalimiana na watu,, kutoonyesha kujali mtu anapopata matatizo na mambo mengine mengi yanayoendana na hayo.

Wewe kwako unaweza ukaona kama  mambo hayo hayana umuhimu sana lakini kumbe yakaja kuwa kikwazo katika maisha yako au mafanikio yako,, fahamu kabisa mtu mwenye dharau asiyejali wengine au asiyejali kusalimia wengine hawezi kuwa na rafiki na kama anafanya hivyo hata kwa ndugu zake wa karibu basi anakuwa kwenye hatari  ya kutengwa,, hata kama umejaliwa kuwa wa tabaka fulani au unajiweza kamwe usidharau wengine na kuwaona hawafai kwasababu huwezi kujua baadaye nini kitatokea kwa ambaye hukumthamini au kumjali na sasa akawa msaada kwako

Hivyo ni vyema kujitafakari na kujiangalia upya kwa kuangalia uhusiano wako muhimu kwa Mungu, mume ama mke wako, watoto , ndugu, wafanyakazi wenzako, na jamii nzima kwa ujumla KAMA UTAGUNDUA KUNA MAMBO ULIKUWA UNAYAPUUZA NA KUONA NI MADOGO JIREKEBISHE KWASABABU YANAWEZA KUKUSABABISHIA MATATIZO MAKUBWA KATIKA MAISHA,,, KWANI MDHARAU MWIBA MGUU HUOTA TENDE,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Maoni 1 :

emuthree alisema ...

ndugu ndugu yangu, mpendwa sana, mdharau mwiba guu huota tende, na mficha uchi hazai, na.....tupo pamoja

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom