Ijumaa, Februari 10, 2012

Kuelekea sikukuu ya wapendanao unaweza kutumia siku hiyo kusherekea na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Pichani ni mwanadada Mange akiwa na watoto yatima ambapo kuelekea Valentine's day ameamua kushirikiana na wadau mbalimbali ili kusherekea pamoja na watoto yatima shughuli hii itakuwa siku ya jumapili tarehe 12,  nimependa sana uamuzi huu jamani kwani hawa watoto wanahitaji misaada na upendo kutoka kwa jamii inayowazunguka ukitaka kufahamu zaidi ingia katika blog ya Mange http//www.u-turn.co.tz
Valentine's day pia unaweza kuwa na yule umpendaye na si kumtafuta siku hiyo kwani kuna wengine wanatafuta wakuwa nao siku hiyo ni bora uwe na marafiki zako au familia yako kuliko kutafuta mpenzi mpya kwaajili ya siku ya wapendanao

Watoto Yatima Pichani TUWAPENDE NA KUWAKUMBUKA KWANI SISI SOTE NI NDUGU.


Maoni 1 :

emuthree alisema ...

Hiyo imekaa vyema mpendwa, sio wapendanao wanakula kuku kwa mrija wakati mayatima, watoto wa mitaani, masikini, wanaishia majalalani...tutalaaniwa jamani!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom