Jumapili, Februari 12, 2012

Rest in Peace Whitney Houston

Whitney Elizabeth Houston alizaliwa tarehe (9 Agosti, 1963  na kifo chake  tarehe 11 Februari, 2012 alikuwa ni mwanamuziki wa Kimarekani, mcheza filamu na mwanamitindo. Whitney ni mshindi wa Tuzo ya Grammy - akiwa kama mwimbaji bora wa pop/R&B, mwigizaji, mtayarishaji wa filamu, mtunzi wa nyimbo na mwanamitindo wa zamani kutoka nchini Marekani.
Alifahamika zaidi kwa kuwa na sauti kali yenye nguvu na mvuto. vilevile watu wengi walimpenda zaidi kupitia nyimbo zake  kama "I Will Always Love You" na "I wanna dance with some body" kutoka katika toleo lake la 'The Star Spangled Banner.'.

Pichani akiwa na binti yake Bobbi Kristina ,,Whitney ni mmoja kati ya wasanii wa kike waliopata mafanikio makubwa kabisa katika medani ya muziki. Moja kati ya albamu zake ambazo zilipata kuwa maarufu zaidi ni The Bodyguard (Kibwagizo bora kwa mauzo bora kwa miaka yote) na ndiyo albamu yake iliyofanya vizuri kupita zote.

Whitney Houston alifariki mnamo tarehe 11 Februari, 2012 katika mazingira ya utata. Mwili wake ulikutwa katika chumba cha hoteli ya Beverly Hilton huko Beverly Hills, California. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi AMEN.


Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

nilikuwa nampenda sana huyo mdada Mungu amlaze mahali pema peponi

Bila jina alisema ...

yaani hayo ni madawa yatakuwa yamemuua tu

Bila jina alisema ...

amen

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom