Jumapili, Februari 12, 2012

"Kutokana na aliyonifanyia inaniuma sana nimemsamehe lakini nashindwa kuwa na upendo kama ilivyokuwa mwanzo naombeni ushauri nifanyeje"

Mambo dada ade, mimi  ni msichana nilikuwa naomba ushauri. nina rafiki yangu ambaye anatoka africa magahribi ninasoma nae nje ya nchi. tuko chuo tunamaliza mwaka wetu wa mwsho. huyu binti ana tabia ya kutokukaa na marafiki kwa muda mrefu kwa sababu ana attitude problem lakini kwa mimi imekuwa tofauti tumeweza kuwa friends tangu 2009.
kulikuwa na visa vingi lakini mimi ni mtu ambaye naweza kuishi na mtu yeyote hata awe na tabia zipi so she respects the fact that i take her shit . ok jambo lenyewe ni hili, huyo rafiki yangu ana boyfriend wake ambaye aliwahi kunitongoza na nikamtolea nje. baada ya hapo akaanza kunichukia sana na kumwambia rafiki yangu asiwe karibu na mimi. 
Kabla ya hilo jambo tulikuwa karibu sana na walikuwa wanapenda sana company yangu so hata tulivyokuwa tukitoka ama weekend nilikuwa naspend kwao. na tulikuwa tunalala kitanda kimoja. . basi baada ya kumtolea nje aliweka kinyongo. weekend moja tulitoka na tuliporudi wakasema kwamba its late ku drive kunirudisha kwangu kwa hiyo nitalala kwao asubuhi watanirudisha. 
Basi nikalala na baada ya muda kidogo yule rafiki yangu akaenda chooni, akiwa chooni huku nyuma  yule boyfriend wake akaanza kunishika makalio nikatoka kitandani na kumkimbia na baadaye yule rafiki yangu akarudi . nilipoamka asubuhi wakanirudisha kwangu. kumbe yule mwanaume alipanga kunifanyia kitu kibaya kupitia rafiki yake. alimpa namba anitongoze alale na mimi na anifanyie kitu kibaya . 
Mimi nikawa nimekasarikia kwa nini ampe namba yule mtu anitake kimapenzi, nikaamua kumuuliza kwanini alimpa namba yule rafiki yake mimi  sio malaya.. basi akakasirika eti kwanini nimemuuliza akamwambia rafiki yangu mambo mengi ya uongo kuhusu hiyo ishu wakati mimi nilimuuliza tu wala sikumtukana . basi wakanishambulia wakanitukana ilikuwa siku ya mwaka mpya.
Nililia sana na niliumia na baadaye yule msichana akaja kuniomba msamaha nimesamehe lakini nimetokea kumchukia ingawa namchekea tu usoni.. naomba ushauri  manake naona moyo unakuwa mzito kuwa na upendo niliokuwa nao mwanzo,..

Maoni 5 :

Bila jina alisema ...

kama umeamua kusamehe ni bora kutokuwa na kinyongo kwasababu utakuwa unajiumiza wewe mwenyewesamehe huku moyo wako ukiwa safi

Bila jina alisema ...

basi wewe ni mnafki ndiyo maana unashindwa kusamehe

Bila jina alisema ...

pole mwayego urafiki ni kazi sana msamehe kiroho safi usifikirie yale mabaya aliyokufanyia wewe fikiria urafiki wenu na umuhimu wake

Bila jina alisema ...

Something wrong with you,it looks cultures different east/west africa playing the roll,you can choose a friend not a relative what are doing at uni idiot!

Bila jina alisema ...

Ilikuweje ukalala kitanda kimoja na rafikiyo pamoja na mpenzi wake? Nimekushangaa mno kwamba kweli ulijikabidhi mikononi mwa simba.yaani rafiki yako na mpenzi wake wakakushawishi ulale nao kitanda kimoja au chumba kimoja?

Hata unaposema alikutongoza ukamtolea nje haiji akilini,bila shaka ulikuwa unamtaka hata wewe.Yaani binti wa Kitanzania umeenda kufanya kioja hicho na unasema eti alikuwa anataka kukufanyia kitu mbaya wakati mwenyewe ulijirahisha kulala nao chumba kimoja na kitanda kimoja!! Sasa unaomba ushauri wa nini wakati unasema umemsamehe si kimbia tu usiwe karibu naye.Mtu kakupangia kukufanyia kitu mbaya na bado unaendelea na urafiki naye karibu?Huo ni unafiki ni afadhali usiwe karibu naye.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom