Katika maisha tunakutana na vitu vingi wakati mwingine vinakupa furaha na wakati mwingine unapata hasira kuna baadhi ya watu anaweza kuwa amekasirika kwa jambo fulani lakini asiseme au kumwambia muhusika ambaye amemkosea ijapokuwa atanyamaza kimya lakini kuna wakati lazima utakuwa na hisia za hasira na utaonyesha hata kwa vitendo unaweza kuonyesha kwa kuwa na chuki au unacheka kinafki lakini pia namna unavyoongea, au kuangalia kwa hisia za hasira NI VYEMA KUWA MUWAZI KWA KINACHOKUKERA KULIKO KUKAA KIMYA KWANI HISIA HAZIJIFICHI NA WAKATI MWINGINE UNABAKI UNAUMIZA MOYO WAKO MWENYEWE. |
Maoni 2 :
Ni kweli ndugu yangu, sema usikike usiwe na donge moyoni, na ni vyema kutafiti ukweli wa jambo, kabla hujafikia maamuzi au sio?
Mie nina tabia hiyo.. yaani sikwambii kama umeniudhi lakini utashaa hayo matendo nitakayokuwa nakufanyia..
Chapisha Maoni