Alhamisi, Februari 09, 2012

"Nimemlipia ada masomo yake ya chuo,,nimemjengea nyumba na kumfanyia mambo mengi ya maendeleo lakini anaolewa na mwanamume mwingine"

Mimi ni mwanamume mkazi wa Morogoro ila kwa sasa naishi Dar es salaam katika maisha yangu nilitokea kumpenda sana dada mmoja ambaye wakati tunaanza mahusiano alikuwa kidato cha sita, baadaye alipomaliza elimu ya sekondari kutokana na wazazi wake kutokuwa na uwezo wa  kumuendeleza  masomo ya chuo nilichukua jukumu hilo mimi,, nakuamua kumlipia ada ya  chuo hadi atakapofikia malengo yake.

Wazazi wake walifurahi sana na walikuwa wanafahamu ni kwa kiasi gani nampenda mtoto wao. maisha yaliendelea yeye alikuwa akisoma chuo Dar es salaam ambapo alinishauri tujenge nyumba ili tuje kuishi pamoja baadaye nilijenga nyumba Dar es salaam  na baada ya kumalizika alihamia na kwenda kuishi huko na hati ya nyumba nilimuachia akae nayo ijapokuwa ilikuwa na jina langu,,

Ukweli ni kwamba nimemfanyia mambo mengi ya maendeleo nikijua kuwa angekuja kuwa mke wangu, tatizo ni kwamba baada ya kumaliza chuo mwenzangu tabia zake zimebadilika hana mapenzi ya dhati kwangu, kilichoniuma zaidi ni siku niliyoenda kumtembelea katika nyumba ambayo mimi ndiye niliyejenga alikuwa akiishi yeye,, niliwahi kumuambia tuishi pamoja akaniambia tufanye hivyo baada ya kufunga ndoa na mimi sikuwa na wasiwasi kwani nilimuamini sana.. 

Siku hiyo nilipoenda kumtembela nilishangaa aliniambia mbona haujanitaarifu, kama unakuja, kumbe alikuwa na mwanamume ndani huyo mwanamume alikuja na kujitambulisha kuwa yeye ni mume mtarajiwa wa huyu dada,, akanionyesha na kadi ya harusi sintosahau iyo siku nilihisi kuchanganyikiwa hata nguvu za kuongea ziliniishia nilishindwa kufanya chochote hadi sasa hivi kazi zangu nashindwa kufanya vizuri.

Sijui nifanyeje nikiwaza hadi kufikia mikakati ya ndoa inamaana huyu msichana pamoja na wazazi wake wote walikuwa wakinitumia?? inaniuma sana sijui nianzie wapi natamni nipate vitu vyangu kama nyumba na gari nilivyompa. naombeni ushauri kupitia blog ya Adela.......

Maoni 17 :

Bila jina alisema ...

Pole sana Brother, wanaume kama wewe ni wachache sana kuwapata kwa siku hizi. Kwa ushauri wangu, this lady is a cruk, na amekutumia bigtime, please the ealier the better, fanya bidii umtoe kwenye nyumba haraka sana. Na huyo mchumba mpiya mjuze kuwa nyumba ni yako na ulikuwa mchumba mtarajiwa; Please nakusihi sana fuatia kilicho chako na mapema, hata ikibidi tumia watoto wa mujini wakusaidie, uwalipe. Utakosa vyote huyu siyo mtu wa kumtegemea.

Wahii wahiii please

Bila jina alisema ...

duh! polesana bro kwa kwel binadamu tunatofautiana sana, yani cjui huyo dada kapata wap ujasiri huo na hata ukija kumuoa hatatulia make keshakuonyesha mapema kabisa. Sikushauri kabisa kuendelea nae japo inauma na ni ngumusana kusahau kutokana na kwamba umekuanae for longtime na kumwamini kabisa kama mkeo mtarajiwa lkn hakuna lisilowezekana chini ya jua bro, kama mshauri alotangulia fanya hima chukua kilichochako huyo dada achana nae kabisa, nadhan hata huyo mwanaume anaetarajia kumuoa hajui ataoa mke wa ainagani huyo dada hatakuja kuwa mama mzuri wa familia hatakidogo, ukifuatilia utajatuambia tu, na c ajabu huyo mwanaume kampendea hiyo nyumba na gari bila kujua ni vya mwanaume mwenzie jamani.......
kweli binadamu tunatofautiana sana!!!

Bila jina alisema ...

POLE SANA KAKA YANGU KAMA HUTOJALI NIPE MOYO WAKO NITAKUPENDA DAIMA HUYO ATAKUJA KULIPA POLE SANA MWAMBIE AKUPE NYUMBA HIYO KAMA KAMKUBALI HUYO MCHIZI WAKE a natakiwa na vitu vyako asivikubali pia komaa upate vitu vyako achana nae huyo siyo mtu hata kidogo hata kulipa fadhila hakuna .weka e-mail yako nikutafute nadhani utanifaa yaani .kakutana na kibaka huyo kamuona kapendeza sana ndo anamtaka wewe subiri kama hawajui wanaume walivyo washenzi ndo atawajua sasa mimi naogopaga sana mtu kunililia jamani mana najua nitalipa yale machozi kama si leo basi kesho yake nitalipa hata kumuumiza mtu siyo jamani dunia hii.mmmh atalipa atarudi huyo kupiga magoti nisamehe dear alafu kuna kuwa hakuna chance ndo atakapojibeba hapo mweee!pole saana eeeeeeeeeeeeeeeeh mpendwa.weka e-mail yako nitakutafuta nitakufariji mimi hapa.achana nae huyo.hamna kitu hapo

Bila jina alisema ...

ATAJUTAJE HUYO KACHEMKA HUYO WANAUME WA HIVYO TUNAWASAKA AF MSHENZI HUYO ANALETA UPUMBAFU ACHANA NAE FANYA UPATE KILICHO CHAKO MJINGA HUYO SOOON OR LATER ATAKUPIGIA MAGOTI NA WAZAZI WAKE HAO WAIT MAISHA YATAPIGA PLUS NA CHOZI LAKO ATAONA DUNIA CHUNGU HII.

Bila jina alisema ...

POLE SANA NAELEWA UNAJICKIAJE SASAHIVI ILA KACHUKUE KILICHO CHAKO KWA MSHAMBA HUYO KAKUTANA NA WATOTO WA MUJINI WANAMDANGANYA TU SUBIRI ATAJUTA SANA WEWE MUACHE TU ..........! UTARUDI HAPA KUSEMA ETI ANAOMBA MSAMAHA ARUDI KAKA HUYO NA USIMPE SECOND CHANCE ATAKUMALIZA ZAIDI FOR SURE SHUKURU MUNGU KWA KILA KITU YAWEZEKANA KAKUEPUSHA NA BALAAA HUKO MBELENI UTAPATA MSICHANA ANAEJUA NINI MAANA YA LOVE NNINI MAANA YA MAISHA HADI UKASEMA HEE MBONA NILICHELEWA KUMPATA HUYU MSICHANA NILIKUWA WAPI.WAPO MABINTI WANAJUA KUPENDA NA KULIPA FADHILA KWAMBA KUWA HIVI NI MUME WANGU AU NI MCHUMBA WANGU KILA LA KHERI PIGA GOTI SHUKURU MUNGU KWA KILA KITU.ANZA UPYA KAKA YANGU UNAWEZA SOON OR LATER MUNGU ATAKUPA MKE MZURI ANAEJUA NINI MAANA YA LOVE NATAMANI NIKUPATE MIE NAWISH HIVYO .

Bila jina alisema ...

HEBU WEKA E-MAIL YAKO NIKUFARIJI KAKA MANA DUH UTAKUWA NA MACHUNGU MNOOOO!

Bila jina alisema ...

POLE SANA MY KAKA MUNGU AKUPE UVUMILIVU UWEZE KUMSAHAU ILA NENDA FASTA KACHUKUE NYUMBA YAKO NA GARI FASTA NENDA WATAFUTE VYA KWAO SIYO WAPANDA MAGRI YA WATU WAKATI MAPENZI HAWATOI NENDA ACHA KUWA NA HURUMA UBAYA UBAYA TU MAISHA HAYA KUWA YESU HAIWEZEKANI JAMNI NENDA KAWATIMUE NA GARI KACHUKUE PIA .NDO WAENDELEE KUPENDANA SASA KAMA KWELI WANAPENDANA UWAONE SASA KAMA HAJARUDI KUSEMA DEAR NISAMEHE TIMUA HUKO MANA NI MTU MZIMA HYO WALIKUWA WANAKUTUMI TU HAKUNA LOVE HAPO YAWEZEKANA ALIYE NAE SASA NDO ANAE MPENDA KWELI AF JAMAA HAMPENDI ANAPENDA MALI ZA DADA HUYO BILA KUJUA KAMA SI ZA DADA HUYO PATAMU HAPO BONGE LA CINEMA HILO.TIMUA CHUKUA MALI ZAKO WATAFUTE WAANZE NA A KAMA WANAPENDANA TUONE AMBACHO HUWEZI KUCHUKUA NI ELIMU YAKE .ILA VINGINE CHUKUA ATAJUTA MAISHA YAKE YOTE .

Bila jina alisema ...

Pole sana kaka yangu kwa mkasa huu ulikukuta lakini cha kufanya put all your Strength together as far as your house and car is on your name as you say it make sure you get it back before its too later because if that cruk will get marriage you will loose what's your so do something fast.

Pia huyo mwanamke na wala wazazi wake wakukupenda wewe bali walikutumia wewe ili waweze kupata wanachokita na walivyopa wakakuacha lakini mungu atakupa wako hujui kakuepushia nini alivyoondoka bora umejua hili kabda hujamuona kuliko ungemuoa halafu ungue kuwa nauhusiano na mwanaume mwingine. pole sana utapata wako anayekupenda, fanya uwezavyo upate vitu vyako vyote kabla hujachelewa.

Bila jina alisema ...

Asanteni sana kwa ushauri wadau wa Adela Blog binafsi nimeshaongea na mwanasheria ameniambia inawezekana kupata vitu vyangu ila bado sijamtoa huyo mwanamke nimeumia sana na sijui kama itatokea nimuamini mwanamke katika maisha yangu sikujua mtu niliyempenda kuliko kitu chochote angenifanyia hivyo tena ananidharau na kunitumia message za kunikebehi huku akiniakikishia nyumba siipati mimi ni mstaarabu sana ila katika hili naamini Mungu atanisaidia nikifanikisha kupata vitu nitawaambia asanteni kwa ushauri nimeamini usilolijua ni usiku wa kiza

Bila jina alisema ...

Hizo pesa ulizipata kifisadi ndio maana hukujali kuzitumia kihivyo.Yaani mimi naamini dalili zilikuwepo tangu awali kuwa huyo bibnti alikuwa nawe kwa kusaidiwa tu.Ungezipata hizo pesa kihalali na kwa jasho la juani ungekuwa makini kwa unayetaka kumsaidia na kuendelea kumtafiti zaidi,lakini wewe ukabweteka hadi nyumba unamwachia na unapomwambia muisho wote anasema hadi muoane, kwani nini kilibaki na amekula kila kitu chako na wote mmedonoana tangu akiwa secondary hadi chuo?

Wanaume wenzangu kuweni makini na wadada wa siku hizi wapo kutafuta miteremko zaidi, ingawa wengine kiukweli hawaangalii pesa bali upendo,lakini wengi wapo viruka njia tu.

Pole sana mdogo wangu,ila usingoje hadi siku zipite kurudisha mali yako kwani utakuta naye kafanya mbinu zingine,fanya fasta sana.

Bila jina alisema ...

pole sana kaka yangu,am speechless...imeniuma sna

Halle alisema ...

HMM! Pole sana kaka! mwanamke gani huyo mwenye tabia za kinyama! mungu atakulipia! anajiona ni mjanja sana! atakuja kkukumbuka muombe Mungu akupe uhai2 na afya njema!

Bila jina alisema ...

SIYO KWELI MDAU JAMNI HIVI UNAJUA KUPENDA INAVYOKUWA AU WASEMA TU KWAMBA HELA ZA KIFISADI KAKA KARIBU TENA UKITAKA USHAURI ACHANA NAE HYO AF SIYO MABINTI WOTE TUKO KIHELA ZAIDI JAMANI MBONA MIE NINA MTU WANGU HANA HATA MIA NANINAMPENDA SANA NA MIMI NDO NAFANYA KAZI YEYE NDO KWANZA ANAKOMAA NA KITABU SO MSIFANYE HITIMISHO KWAMBA WOTE NI VICHECHE TU AF KAKA USIJALI UTAPATA TU BINTI ATAKAYEKPENDA ILA USIENDE KICHWA KICHWA IKIWEZEKANA JIFANYE HUNA HATA MIA MBELE YA SAFARI NDO UMUONYESHE KWAMBA SI KWELI UNAZO KILA LA KHERI MPENDWA KATIKA BWANA AU MTUME.

Bila jina alisema ...

NO MATTER WHAT!!!! LET IT GO BRO. KWENYE MAISHA UNAWEZA KUFANYA BIASHARA NA USIPATE FAIDA. HIYO ILIKUWA NI BIASHARA LAKINI HAIKUKUPA FAIDA. SONGA MBELE MAISHA BADO YAPO NA LAZIMA YAENDELEE

Bila jina alisema ...

pole kaka yangu kwani hata mimi yamenikuta kama yako, kama vip nipe email yako nikutafute ili tufarijiane

Bila jina alisema ...

Pole but jifunze kuanzia hapo, never practise "in marriage" wakati hujaoa, mwishowe utaumizwa kama ulivyofanyiwa, maana si kila unaye date naye basi utamuoa, la hasha. But mali zako unaweza kudai hasa zile ambazo hamkushirikiana kuzitafuta"JOINT EFFORT", Kusoma na vitu vingine nifaida yake ya kudate nawewe, atakumbukia.... Please guys kuweni makini ni vijitabia ambavyo vimezuka mijini, kuhitana WIFE, HUSBAND, kufuriana nguo, kupikiana vyakula, Kulipiana ada za shule, kama utafanya ujue vikigeuka utakuwa cross yako.

Bila jina alisema ...

Pole but jifunze kuanzia hapo, never practise "in marriage" wakati hujaoa, mwishowe utaumizwa kama ulivyofanyiwa, maana si kila unaye date naye basi utamuoa, la hasha. But mali zako unaweza kudai hasa zile ambazo hamkushirikiana kuzitafuta"JOINT EFFORT", Kusoma na vitu vingine nifaida yake ya kudate nawewe, atakumbukia.... Please guys kuweni makini ni vijitabia ambavyo vimezuka mijini, kuhitana WIFE, HUSBAND, kufuriana nguo, kupikiana vyakula, Kulipiana ada za shule, kama utafanya ujue vikigeuka utakuwa cross yako.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom