Jumatatu, Machi 05, 2012

Inapendeza mtoto kupata malezi ya baba na mama

Ni wazi kabisa inapendeza sana mtoto kupata malezi ya baba na mama, siku hizi kuna baadhi ya kina dada wanasema "Mimi kuolewa siolewi bora nizae mtoto wangu nimlee mwenyewe" Ukweli ni kwamba kwa aslimia kubwa unakuta wanawake wengi wamezaa watoto lakini wanawalea wenyewe ama unakuta analelewa na baba , bibi, shangazi nk. Lakini pia wapo ambao unakuta wanafanya hivyo kutokana na matatizo fulani ambayo yapo nje ya uwezo kama migogoro katika mapenzi, kutengana, kifo nk.

Ni vyema kuwa na malengo mazuri ya kuishi na kulea mtoto kwa ushirikiano wa baba na mama. Kila mmoja ashiriki kikamilimu katika malezi ya mtoto. Inakera baba au mama kumtenga mtoto wake bila ya kuwa naye karibu kwa malezi na makuzi. Vilevile kwa watoto ambao hawana wazazi wanahitaji faraja kutoka kwa walezi na upendo kama ilivyo kwa wale wanaolelewa na wazazi wao.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom