Jumanne, Machi 06, 2012

Ni vyema Kujitambua na kuishi kama ulivyo

Katika  maisha ni vyema sana kujitambua na kuishi kama ulivyo, ni wazi kabisa binadamu tumeumbwa na tabia tofauti, lakini ukijitambua basi utajikubali na kujua nini ufanye katika maisha yako  na unaweza kuishi vizuri kuliko kujiingiza katika matatizo ama shida ambazo zinaweza kukukumba kwasababu ya kutaka kuishi maisha kama ya mtu  fulani au mtu mwingine, wapo watu hawalali wapo radhi kuiba, kufanya ukahaba alimradi awe na maisha kama ya fulani, kama fulani ana gari au nyumba ya kifahari isiwe kwako tatizo na kujiona kama maisha haujayapatia maana huwezi kujua mwenzio amepata kwa njia gani. jitambue na ongeza juhudi katika kazi yako na utafikia malengo yako ni mbaya sana kulazimisha kufanya jambo bila juhudi.

Haikatazwi kuwa na matamanio lakini yatafute kwa njia zako kama ni kusoma, kuanzisha biashara na njia nyingine nzuri za kujikwamua lakini sio kutaka kile alichokuwa nacho mwenzako  basi na wewe lazima uwe nacho. Lazima ujitahidi kuishi maisha ya kujiamini na kujikubali na kuamini kwamba unao uwezo wa kufanya jambo fulani na kutimiza ndoto yako.

Kuna baadhi ya watu  wanaiga hata akiona mwenzie kaolewa ama ameoa basi na yeye anataka kuwa hivyohivyo bila kujua mwenzie alijipanga vipi na kuamua kuingia kwenye ndoa. mwisho wa siku kutokana na kukurupuka bila kujipanga ndoa inashindwa kudumu. tusifanye mambo kwa kuiga ni muhimu sana kujitambua.

JIPENDE MWENYEWE KABLA HAUJAPENDWA ...JIKUBALI NA JITAMBUE

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Ni kweli wengi hatujitambui ila kupitia hii post uliyoiweka najua kila atakayesoma hata baki kama alivyokuwa mwanzo ni hakika tumebadilika na fikra chanya tulizokuwa nazo. Mada nzuri Be blessed

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom