Jumatano, Aprili 25, 2012

ADELA VOICE SIKU YA LEO sikiliza mkasa huu kwa umakini yaliyomkuta Sarah katika familia yake amegundua rafiki yake anatoka kimapenzi na baba yake mzazi sikiliza kisa hicho nimekisimulia kwa umakini,,,


Maoni 7 :

Bila jina alisema ...

Nimekipenda sana hiki kipengele Adela yaani inasikitisha sana mimi namshauri Sarah amuambie ukweli mama yake au atafute mtu mzima akamweleze

lyna wa ukweee alisema ...

namshauri sara amwambie mama mna akikaa kimya inaweza kumcost badae,mna uwez jua hapo kma baba ake uko aendako ana tumia kinga au lah asije mkosa mama bure kwa hupuz wa baba ake!na uyu rfk yake awez kuwa na uyo baba peke yake lzma ana mtu mwingne.na ndo hapo ukimwi unapotambaa

mammy alisema ...

yaani imenisikitisha sana sijui sisi wanawake tuna matatizo gani?Sara amwambie mama yake tena kwa mimi ningemwambia mbele ya baba wakiwa pamoja kwani akiliweka moyoni litamuathiri Sara baadae.na hata ktk masomo hatoweza kuyamudu vizuri.

Elsa alisema ...

Pole sana kwa sara ila mie namshauri atafute mtu mzima huko kwao, au mtu anayemwamini aweze kuongea nae kwanza pili wamwendee baba na kumuonya kuhusu kuacha hiyo batia ikishindakana ndio mama aambiwe.. Wazee wengine bwana pyuuuuuu aibu tupu.

Bila jina alisema ...

imeniudhunisha sana Adela huyo dada atafute njia ya kumwambia mama yake ukweli

Bila jina alisema ...

hongera Adela kwa kipengele hiki nimekipenda sana nitakuwa nakifuatilia sana pole sana Sara Mwambie mama yako usikae kimya

Bila jina alisema ...

Ukijaribu kuliangalia suala hilo kwa mapana kiasi utagundua kwamba si sahihi kama huyo Sara atakwenda moja kwa moja kumuambia mama yake, kwani madhara yake yatakuwa makubwa sana.
Kuna uwezekano mkubwa sana baba yake sara akawa ametumia udhaifu wa huyo rafiki yake na sara kumshawishi kimapenzi na huyo binti shida na tamaa zinapelekea yeye kuingia huko.
Wala asikimbilie kupeleka habari nje yeye ni mtu mzima anaweza kueleza hisia zake kwa baba yake na kama baba ni mwelewa ataacha.Sina maana ya kumtetea huyo mzee ila naamini Sara anauwezo wa kulikemea jambo kwa kutumia busara sio hasira.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom