Karoti inaweza kuliwa mbichi, kupikwa na kuchanganywa na mbogamboga, kutengenezwa saladi na juisi. Faida zinazopatikana kutokana na utumiaji wa karoti ni kuongeza vitamini “A” ambayo inatokana na beta-carotene iliyomo ndani ya karoti na pia huongeza vitamini B, C, E na madini ya chuma mwilini.
Karoti ina protini kidogo na haina mafuta ukilinganisha na mazao ya jamii ya kunde na yenye asili ya uwanga. Vile vile karoti ina nyuzi nyuzi (fiber) ambazo ni muhimu kwa kukinga kuta za utumbo na kulainisha choo. Karoti inasaidia kuongeza nuru ya macho, kukinga maradhi ya ngozi, magonjwa yenye asili ya kansa na kupunguza tindikali inayodhuru tumboni. | |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni