KITABU MALIPO NI HAPAHAPA
ILIPOISHIA..............Baada ya wiki kadhaa kupita mawasiliano kati ya James na Esta yalikwisha kwani kila Esta alipojaribu kupiga simu James alikuwa hapokei. Na ikitokea amepokea alimtaka asiendelee kumpigia simu tena. Upendo aliondoka na kwenda Morogoro kwa ajili ya kuandaa sherehe. Akiwa Morogoro mdogo wake alikuwa bado yupo chuoni, hivyo wazazi wake walimpigia simu na kumwambia ni lazima awepo kwenye sherehe ya dada yake.
INAPOENDELEA........
Zikiwa zimebaki kama wiki mbili kufanyika sherehe ya kumuaga Upendo,
Eliza alirudi Morogoro kwa wazazi wake ili kusherekea pamoja na dada yake. Siku
Eliza alipofika, wazazi wake hawakuwepo ila Upendo pekee. Upendo alipomwona
mdogo wake alifurahi sana, alimpokea begi wote wakaingia ndani.
“Jamani hatujaonana siku nyingi sana my
young sister (mdogo wangu) mbona umenenepa hivyo ulikuwa unasoma kweli wewe?”
Alisema Upendo.
Eliza alimwangalia sana dada yake:
“Dada Upendo kuna kitu nataka nikwambie, ila iwe siri yako sitaki mama
wala baba wafahamu hili.“ Aliongea Eliza kwa kusihi.
Upendo alishtuka na kuwaza moyoni mwake: “Je, atakuwa ana tatizo gani?”Aliwaza
Upendo. Hebu niambie tafadhali.
“Upendo mwenzio nina mimba hapa
nilipo ndio maana unaniona nimenenepa.” Alianza kueleza Eliza.
“Acha utani wako wewe una mimba ya nani.” Upendo alihoji kwa mshangao.
“Nina mimba ya kijana mmoja
anaitwa Juliasi sijui hata nitampatia wapi najua anakaa Dar es salaam, lakini
sijui nitaanzia wapi kumpata.” Alisema Eliza huku akiwa ameinama.
“Inamaana wewe umepata mimba ya
mtu ambaye hata ha umjui vizuri, kweli mdogo wangu umechezea maisha yako.”
Aliongea Upendo kwa kejeli.
Eliza machozi yakiwa yanamtoka,
“Nisaidie dada yangu mimi sijui
nifanyeje hapa nilipo kwani hata mwanamume mwenyewe nikimpigia simu hapokei na
ameshakataa hii mimba ameniambia niitoe na mimi siwezi kufanya hivyo”.
“Haiwezekani! Hiyo mimba usitoe kumbuka
nilikuonya mdogo wangu uwe makini na hawa wanaume. Wengi wao ni matapeli sasaa…
ngoja, tutajua cha kufanya kesho lakini
usijali sana kwani tayari jambo limetokea, kulia siyo sulihisho.” Aliendelea
kumbembeleza na baadaye alimtaka akaoge ajiandae kwani wazazi wao wangerudi
muda huo.
Wazazi wao walikuwa wamekwenda kuwachukua ndugu wengine, lakini walikuwa
wanafahamu kuwa Eliza anakuja siku hiyo. Baada ya dakika kadhaa kupita wakiwa
wanaendelea na mazungumzo Baba na Mama yao pamoja na ndugu wengine walifika. Upendo
aliwakaribisha wageni, na kuwaelekeza sehemu za kukaa.
“Karibuni sana, wengine wakae pale na wengine hapa, waswahili husema ‘sherehe ni watu’, na watu wenyewe ni ninyi,
sisi na wengine watakao kuja.” Upendo aliwaelekeza wageni. Baba Upendo (Mzee
George) alimtuma Upendo akamwite mdogo wake aje awasalimie wageni. Upendo
aliinuka haraka na kuelekea chumbani.
“Eliza unaitwa na baba ili ukawasalimie baba, mama na wageni. Nakuomba
uvae gauni kubwa ili wasielewe mabadilko uliyonayo, kwani mimba uliyokuwa nayo imeanza
kujionyesha.” Alishauri Upendo.
Eliza alijiandaa kama alivyoshauriwa na Upendo kisha wote wakaelekea
sebuleni. Alipofika aliwasalimia wazazi na
shangazi yake na wageni wengnie waliokuwepo
”Jamani ni wewe wajina wangu Esta umekuwa mkubwa hivi”. Shangazi yake
alishangaa kuona Eliza amekuwa mkubwa.
“Yaani dada, hilo jina la Esta mwenzio halitumii anatumia jina la Eliza,
wamekuwa wakubwa sana. Hata sisi hatujawaona siku nyingi. Huyu yupo chuoni Arusha
anaingia mwaka wa mwisho.“ Alifafanua Baba Upendo huku akimwangalia shangazi
yake Eliza na kucheka.
“Kweli siku zinakimbia na hilo jina la Esta ha ulitumii unapenda kuitwa
Eliza mama jamani watoto wa siku hizi.” Aliendelea kushangaa na kucheka
shangazi yake Eliza.
“Hapana shangazi, huwa nalitumia
mara moja moja.” Alijibu Esta huku akiinamisha kichwa chini kwa aibu.
“Lakini bora usilitumie kwani haya majina ya kurithi wakati mwingine sio
mazuri unaweza ukampa mtoto jina la mtu mwenye mikosi na mtoto akajikuta
anakuwa na mikosi katika maisha kwa sababu ya majina ya kurithi.” Alisema
shangazi yake huku watu wote wakiangua vicheko.
“Hakuna wifi hizo ni imani tu za
watu.” Alijibu mama Upendo huku akiinuka kuelekea jikoni.
“Haya jamani huku jikoni vipi?” Aliuliza mama Upendo.
“Tayari mama hakuna tatizo.” Alijibu Upendo.Nini kitaendelea usikose sura ya 9..................
Maoni 5 :
mhhhhhhhhhhhh yesu sipt pic james akija hapo,duh inanoga
jmn mbona najarb ku click read more yagoma mpz?
adela read more haifunguki
Ok naona mimi nikifungua inafunguka ngoja nijaribu kuweka sawa wadau tuko pamoja sana
jamani yunasubiri hiyo sura ya 9 mbona unatukosesha utamu adela
Chapisha Maoni