KITABU MALIPO NI HAPAHAPA
Kwa wadau mbalimbali wa simulizi zangu na ambao wanahitaji kitabu kilichosheheni simulizi za kusisimua sasa kinapatikana mkoa wa Mwanza, Kahama, Tabora, Musoma na Dodoma
Mwanza kinapatikana BOOKPOINT karibu na kituo cha mafuta TRA zamani
Kahama kinapatikana MUSHI STATIONARY ipo karibu na stendi ya mabasi
Musoma kinapatikana Musoma mjini kwa muuza MAGAZETI stendi ya zamani ya mabasi
Tabora kinapatikana URAMBO mjini SIZANI Bookshop kwa Shekhe Bilali na Barabara ya Salmini karibu na Meya Hotel CHABRUMA duka la vitabu bado naendelea kusambaza mikoa yote tutaelekea ARUSHA,MBEYA,MOSHI ,TANGA NK...
SURA YA KWANZA SIMULIZI YA MAMA MDOGO
Jamali
ni kijana ambaye amezaliwa katika familia ya watoto wawili akiwa ni mtoto wa
kwanza. Ana mdogo wake ambaye ni msichana.
Katika maisha yao wameishi katika mazingira mazuri kwani mama yao
alikuwa na uwezo mkubwa sana kifedha na aliwapa kila walichokihitaji.
Baada ya mama yao mzazi kufariki na kuwaacha na baba yao Mzee Said
ambaye alikuwa akimiliki mali zote baada ya kifo cha mke wake. Mzee said baada
ya muda kupita aliamua kuoa mwanamke mwingine ambaye alikuwa na rika moja na
mwanawe Jamali.
Mkoa wa Dar es salaam ni mkoa ambao umejaa wakazi wengi kutoka maeneo
mbalimbali nchini Tanzania na pia kumesheheni wafanyabiashara mbalimbali
wakubwa kwa wadogo. Maeneo ya Masaki katika Mkoa wa Dar es salaam ni sehemu
ambayo wanaishi watu ambao wana uwezo sana kifedha na kuna utulivu pamoja na
ulinzi mkali sana maeneo hayo.
Familia ya Mzee Said ni moja kati ya wakazi waliokuwa wakiishi katika
maeneo hayo akiwa pamoja na mke pamoja na watoto wake Jamal na Aisha. Mama
Jamal alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa sana akiwa anajishughulisha na kampuni
zake binafsi katika uuzaji wa vifaa vya ujenzi na pembejeo akisaidiana na mume
wake Mzee Said.
Mzee Said alikuwa akifanya kazi katika Wizara ya Kilimo, na watoto wao
walikuwa wakisoma katika shule nzuri sana. Jamal alikuwa Kidato cha Kwanza na alikuwa
akisoma shule ya kutwa, wakati Aisha alikuwa akisoma Darasa la Pili. Jamal na
Aisha waliishi kwa kupendana na mara nyingi walikuwa wakicheza pamoja. Kwa
ujumla maisha katika familia ya Mzee Jamal yalikuwa mazuri yenye amani na
upendo siku zote.
Jamal alipofika Kidato cha Tatu mama yake alitaka akasome Mkoa wa Kilimanjaro
katika shule za bweni ili apate muda mwingi wa kujisomea. Aliamua kumwambia Mzee
Said juu ya wazo lake, kabla ya kumwambia Jamal. Ilikuwa ni jioni wakati Mzee Said na mkewe wakiwa wamekaa katika uwanja wa nyumbani kwao. Jamal na
Aisha walikuwa wakibembea huku wazazi wao wakiwaangalia.
"Baba Jamal hivi unaonaje tungempeleka Jamal katika shule ya bweni
ili apate muda wa kutosha wa kujisomea.” Alishauri mama Jamal.
“Hapana naona hujawaza vizuri. huoni
kama Aisha atakuwa mpweke kwani amemzoea sana kaka yake. Mimi sijaona tatizo hata akisoma tu hapahapa hata hivyo mbona
shule anayosoma ni nzuri sana!” Mzee Jamal alichangia mada ingawa alikwenda
kinyume na wazo la mkewe.
“Sawa mume wangu ila hata kama ni hapahapa Dar es salaam akalale hukohuko
shuleni ili aweze kupata muda wa kujichanganya na wenzake katika kujisomea
kuliko kwenda na kurudi.” Alisisitiza
mama Jamal.
“Haya mama watoto hilo halina shida ngoja nimwite Jamal tumwambie.” Alisema
baba Jamal.
“Jamal!” Aliita Mzee Said.
”Naam baba!” Aliita Jamal.
“Hebu njoo!” Aliita Mzee Said.
“Nakuja baba!” Alisema Jamal huku akimshika mkono mdogo wake na kuelekea
waliko kaa wazazi wao.
“Na nyie mnavyofuatana kama
kumbikumbi.” Alitamka mama Jamal huku akitabasamu.
“Kaeni chini basi”. Alitamka baba Jamal huku akimshika Aisha mkono.
“Tumejadiliana na kukubaliana na baba yako kwamba kuanzia wiki ijayo Jamal
utakuwa unalala shuleni ili usome zaidi, kwani tumegundua kwamba huku nyumbani hupati
muda mzuri wa kujisomea.” Alimaliza kuongea mama Jamal.
“Hapana mama mimi nitabaki na nani? Sitaki kama ni hivyo bora na mimi
nikalale shule” Alijibu Aisha huku akimwangalia mama yake kwa hasira. Nini kitaendelea usikose sura ya 2
Maoni 1 :
jmn ongera dada kwa hadithi zako nzuri.
Chapisha Maoni