Jumatatu, Aprili 16, 2012

Umelala usiku mwenzio anachati au anatumia muda huo kuongea kwenye simu na mpenzi wake wa nje je wewe utafanyaje??

Inawezekana mambo haya kutokea  kwasababu ya baadhi ya watu kukosa uaminifu embu fikiria umelala usiku mara ghafla unamkuta mwenza wako anazungumza katika simu na mtu mwingine huku ikionyesha kabisa kwamba ni mpenzi wake au alikuwa anachati ukashtuka na kuangalia simu yake kisha unakutana na ujumbe "Usijali  mpenzi nakupenda sana yaani nakukumbuka sana mambo yako matamu hapa naona usiku mwingi yaani nakutamani sana tamu ya moyo wangu" unakutana na ujumbe kama huu je utachukuahatua gani???  

Ukweli ni kwamba binadamu yeyote ukikutana na hali kama hii utaumia sana mwingine atalia, kudai talaka,kupigana lakini mwingine atakaa kimya huku akilia moyoni mwake. unadhani nini kifanyike inapotokea hali hii,,,,,,,,,,,,,

Maoni 2 :

emuthree alisema ...

Labda na yeye anatafuta usingizi...ni vyema pia kujitahidi kusaidiana kurtafuta usingizi, usikimbilie kulala...ili usimpe nafasi mwenzako kutafuta visingizio

Bila jina alisema ...

yaani tunapigana kwakweli

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom