Mkulima wa kijiji cha Bugenika kata ya Farkwa Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Kingula Mdaki mwenye umri wa miaka 56 anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wake, Kamanda wa Polisi mkoani hapo Stephen Zelothe amemtaja marehemu kuwa ni Kamuya Kingula mwenye umri wa miaka 33 na kwamba alifariki dunia wakati akitibiwa majeraha katika hospitali ya wilaya hiyo.
Amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni ulevi alifafanua kuwa kabla ya tukio hilo marehemu alikuwa anakunywa pombe na mtuhumiwa ndipo wakaanza kurushiana maneno na hatimaye kupigana, amesema mtuhumiwa huyo alimpiga marehemu kwa mkuki sehemu ya kichwani na kusababisha majeraha katika upande wa kisogoni.
Baada ya kujeruhiwa kijana huyo alipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kondoa lakini alifariki dunia akiwa anaendelea na matibabu. Mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili
CHONDE CHONDE ULEVI NI NOMA
Maoni 1 :
TUWEKEENA PICHA DADA ADELA BASI
Chapisha Maoni