KITABU MALIPO NI HAPAHAPA
MTUNZI ADELA DALLY KAVISHE
LIPOISHIA,,,,,
“Lakini bora usilitumie kwani haya majina ya kurithi wakati mwingine sio
mazuri unaweza ukampa mtoto jina la mtu mwenye mikosi na mtoto akajikuta
anakuwa na mikosi katika maisha kwa sababu ya majina ya kurithi.” Alisema
shangazi yake huku watu wote wakiangua vicheko.
“Hakuna wifi hizo ni imani tu za
watu.” Alijibu mama Upendo huku akiinuka kuelekea jikoni.
“Haya jamani huku jikoni vipi?” Aliuliza mama Upendo.
“Tayari mama hakuna tatizo.” Alijibu Upendo.
INAPOENDELEA,,,,,Waliendelea na mazungumzo pale sebuleni na baadaye baada ya kupata
chakula cha usiku wote walikwenda kupumzika. Hatimaye siku ya sherehe ilifika,
sherehe, iliandaliwa pale nyumbani kwa kina Upendo. Kulikuwa na uwanja mkubwa
ambao ulipambwa vizuri sana. Ama kweli ilikuwa ni siku ya furaha kwa Upendo.
Kwa upande wa mdogo wake Eliza
mambo hayakuwa mazuri kwani muda wote alikuwa akiwaza sana kuhusu Juliasi kwa
nini hapokei simu yake.
“Eliza hii ni siku ya furaha ya
maisha yangu naomba uwe na furaha mdogo wangu. Halafu leo pia ni siku mwafaka
kwa wewe kumwona shemeji yako ambaye hujawahi kumwona, nadhani utampenda kwani
nampenda sana.” Upendo alimfariji mdogo wake huku akimpigapiga mgongoni na kiganja
cha mkono wake wa kulia.
“Nitafurahi sana kumfahamu shemeji yangu nadhani alikuwa akinisikia tu.”
Kwa tabasamu la upole Eliza alimjibu dada yake.“
“Ndiyo nilikuwa nikimsimulia sana kuhusu wewe mdogo wangu kwamba upo
chuoni kwa hivyo leo mtafahamiana au siyo mdogo wangu.” Alisema Upendo.
“Asante nitashukuru sana kumwona shemeji, sijui atavaa suti, jinsi na
tisheti au atakuwa katika pamba za namna gani.” Aliongea Eliza huku akitabasanu
na kumwangalia dada yake Upendo.
Mipango iliendelea na hatimaye sherehe ilikaribia kuanza. James na
wazazi wake walitokea hotelini na kuelekea nyumbani kwa akina Upendo maeneo ya
Kihonda ambapo sherehe ilikuwa ikifanyika. Walipofika walipokelewa kwa
vigelegele na shangwe nyingi walipelekwa sehemu ya kukaa na baadaye James
alifichwa katika umati wa watu ili Upendo aje kumtafuta. Upendo alitoka ndani
huku matarumbeta yakipigwa na shangwe nyingi zikitawala akiwa sambamba na mdogo
wake Eliza.
Upendo akiwa sambasamba na Eliza alielekea sehemu ile kwenye umati wa
watu ambako James alifichwa ili akamfichue.
James akiwa katikati ya umati alimwona Upendo akiwa anatoka na pembeni
akiwa na Esta alishtuka sana kumwona Esta.
“Mungu wangu yule si Esta? Anafanya nini hapa na mbona yupo karibu na
Upendo? Kuna nini kinaendelea hapa?” James aliwaza na kujiuliza maswali mengi yaliyokosa
majibu.Nini kitaendelea sura ya 10.......
Maoni 5 :
uwiiiiiiiiiiii ngoma inogile,cpati pic kma c nega!!tufanyie kila bada ya ck mbili jmnmpendwa.
dah sijui jemsi atafanya nini maskini, lakn ndiyo akome hakua mwaminifu kwa upendo.
hi, adela,hapo patamu sasa tulipofika wewe mkali cster,tunashukuru kwa kusikiliza na kutekeleza maombi yaetu mungu azidi kukujalia na kukupa afya njema kila iitwapo leo ,ili tuzidi kupata story zako humu ndani maana.........
Duuuuu, hii stori inanogaje? jamani naomba uwe unatuwekea walao kwa wiki mara mbili, penda ww mdada kazi nzuri
Safi sana Adela stori nzuri sana tuwekee walao kwa wiki mara tatu, ila umetuachia patamu balaaaaaaa
Chapisha Maoni