Ijumaa, Mei 18, 2012

SIMULIZI YA DADA YANGU SURA YA ....9,,,,,


KITABU  MALIPO NI HAPAHAPA 
MTUNZI  ADELA DALLY KAVISHE

LIPOISHIA,,,,,
“Lakini bora usilitumie kwani haya majina ya kurithi wakati mwingine sio mazuri unaweza ukampa mtoto jina la mtu mwenye mikosi na mtoto akajikuta anakuwa na mikosi katika maisha kwa sababu ya majina ya kurithi.” Alisema shangazi yake huku watu wote wakiangua vicheko.
 “Hakuna wifi hizo ni imani tu za watu.” Alijibu mama Upendo huku akiinuka kuelekea jikoni.
“Haya jamani huku jikoni vipi?” Aliuliza mama Upendo.
“Tayari mama hakuna tatizo.” Alijibu Upendo.

INAPOENDELEA,,,,,Waliendelea na mazungumzo pale sebuleni na baadaye baada ya kupata chakula cha usiku wote walikwenda kupumzika. Hatimaye siku ya sherehe ilifika, sherehe, iliandaliwa pale nyumbani kwa kina Upendo. Kulikuwa na uwanja mkubwa ambao ulipambwa vizuri sana. Ama kweli ilikuwa ni siku ya furaha kwa Upendo.

 Kwa upande wa mdogo wake Eliza mambo hayakuwa mazuri kwani muda wote alikuwa akiwaza sana kuhusu Juliasi kwa nini hapokei simu yake.
 “Eliza hii ni siku ya furaha ya maisha yangu naomba uwe na furaha mdogo wangu. Halafu leo pia ni siku mwafaka kwa wewe kumwona shemeji yako ambaye hujawahi kumwona, nadhani utampenda kwani nampenda sana.” Upendo alimfariji mdogo wake huku akimpigapiga mgongoni na kiganja cha mkono wake wa kulia.
 
“Nitafurahi sana kumfahamu shemeji yangu nadhani alikuwa akinisikia tu.” Kwa tabasamu la upole Eliza alimjibu dada yake.“
“Ndiyo nilikuwa nikimsimulia sana kuhusu wewe mdogo wangu kwamba upo chuoni kwa hivyo leo mtafahamiana au siyo mdogo wangu.” Alisema Upendo.
“Asante nitashukuru sana kumwona shemeji, sijui atavaa suti, jinsi na tisheti au atakuwa katika pamba za namna gani.” Aliongea Eliza huku akitabasanu na kumwangalia dada yake Upendo.

Mipango iliendelea na hatimaye sherehe ilikaribia kuanza. James na wazazi wake walitokea hotelini na kuelekea nyumbani kwa akina Upendo maeneo ya Kihonda ambapo sherehe ilikuwa ikifanyika. Walipofika walipokelewa kwa vigelegele na shangwe nyingi walipelekwa sehemu ya kukaa na baadaye James alifichwa katika umati wa watu ili Upendo aje kumtafuta. Upendo alitoka ndani huku matarumbeta yakipigwa na shangwe nyingi zikitawala akiwa sambamba na mdogo wake Eliza.

Upendo akiwa sambasamba na Eliza alielekea sehemu ile kwenye umati wa watu ambako James alifichwa ili akamfichue.  James akiwa katikati ya umati alimwona Upendo akiwa anatoka na pembeni akiwa na Esta alishtuka sana kumwona Esta.
“Mungu wangu yule si Esta? Anafanya nini hapa na mbona yupo karibu na Upendo? Kuna nini kinaendelea hapa?” James aliwaza na kujiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu.Nini kitaendelea sura ya 10.......

Maoni 5 :

lyna wa ukweee alisema ...

uwiiiiiiiiiiii ngoma inogile,cpati pic kma c nega!!tufanyie kila bada ya ck mbili jmnmpendwa.

neema alisema ...

dah sijui jemsi atafanya nini maskini, lakn ndiyo akome hakua mwaminifu kwa upendo.

DAVID JERMOS alisema ...

hi, adela,hapo patamu sasa tulipofika wewe mkali cster,tunashukuru kwa kusikiliza na kutekeleza maombi yaetu mungu azidi kukujalia na kukupa afya njema kila iitwapo leo ,ili tuzidi kupata story zako humu ndani maana.........

Bila jina alisema ...

Duuuuu, hii stori inanogaje? jamani naomba uwe unatuwekea walao kwa wiki mara mbili, penda ww mdada kazi nzuri

Bila jina alisema ...

Safi sana Adela stori nzuri sana tuwekee walao kwa wiki mara tatu, ila umetuachia patamu balaaaaaaa

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom