MTUNZI: ADELA DALLY KKAVISHE
KITABU MALIPO NI HAPAHAPA KIPO MTAANI KWA SASA
EMAIL kavisheadela@yahoo.com
+2550652343430
ILIPOISHIA....“Usijali kuhusu hilo mpenzi, kwani mimi nilichoamua hakuna anayeweza
kunipinga. Wewe ndiye utakuwa mama mwenye nyumba kuanzia sasa. Hapa ni kwako
sawa mamaaa?” Alisema Mzee said kwa kujiamini huku akicheka.
INAPOENDELEA...Mzee Said aliamua kumtembeza Sophia pale nyumbani na kumwonyesha
mazingira yote. Tangia siku ile Sophia aliishi na Mzee Said kama mke na mume na
aliponogewa na mapenzi ya mke mpya aliamua kufunga ndoa harakaharaka bomani
tena kisiri bila watu wengine kujua.
********
Siku moja Jamal aliomba ruhusa kwa mwalimu ili aende Hospitali kutokana
na kusumbuliwa na homa. Baada ya
kuruhusiwa aliamua kwenda nyumbani ili akamtaarifu baba yake juu ya kuumwa
kwake na kisha ampeleke hospitali. Ilikuwa ni siku ya Jumamosi, Jamal alijua
lazima atamkuta baba yake nyumbani. Alipofika na kuingia getini, aliona gari la
baba yake likiwa limepaki. Jamal alifurahi sana kwani alikuwa na uhakika kuwa
baba yake yupo.
“Afadhali nimemkuta baba.” Aliwaza Jamal na kugonga mlango.
Baada ya kugonga mara kadhaa na kukosa majibu aliamua kuingia ndani na
kuanza kuita.
“Baba! Baba!” Aliita Jamal lakini hakupata jibu.
Wakati huo baba yake alikuwa chumbani amepumzika na Sophia. Baadaye Mzee
Said alisikia sauti ya Jamal ikiita kutoka sebuleni, alitoka haraka kuelekea sebuleni
na kumkuta Jamal.
“Hujambo Jamal! Vipi mbona uko hapa shule imefunga?” Alisalimia na
kuuliza Mzee Jamal.
“Sijambo baba shikamoo! Shule hatujafunga ila nimekuja hospitali
nasumbuliwa na homa.” Alijibu Jamal. Kisha baba yake alimsogelea na kumshika
mkono.
“Pole sana mwanangu, sasa umekwenda hospitali?” Aliuliza Mzee Said.
“Hapana baba ndo nimekuja ili unipeleke hospitali.” Alisema Jamal.
“Sawa hebu nijiandae ili twende.” Alishauri Mzee Said.
Wakiwa wanaendelea na mazungumzo mara Sophia alitoka chumbani.
“Vipi darling {mpenzi} kuna mgeni?.” Aliuliza Sophia huku akimwangalia
Jamal.
“Baba kwani huyu ni nani?” Aliuliza Jamal huku akimwangalia Sophia kwa
uso wa mshangao.
“Ahaa, imekuwa vizuri sana mwanangu umekuja ili uweze kumfahamu mama
yako mdogo.” Alijibu Mzee Said huku akigeuka kumwangalia Sophia, ambaye muda
wote alikuwa akitabasamu.
“Mama yangu mdogo? Kivipi baba?”
Alihoji Jamal.
“Ndiyo mwanangu huyu ndiye
atakuwa mama yenu mdogo kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali hapa nyumbani
ikiwa ni pamoja na kuwatunza ninyi.” Alieleza Mzee Said.
Jamal alinyamaza kimya kwa muda huku akimkodolea macho yule binti bila
kusema kitu.
”Hivi huyu Baba ana matatizo gani? Huyu msichana si sawa tu na binti yake?
Haya ni mambo ya ajabu sana. Kamwe siwezi hata siku moja kumheshimu mwanamke wa
umri kama huu kuwa mama yangu.” Aliwaza Jamal.
“Mwanangu sasa nadhani mtafahamiana vizuri na mama yako kadiri siku
zinavyozidi kwenda.” Alitamka Mzee Said.
“Mama yangu! Huyu hawezi kuwa mama yangu hata siku moja. Mama yangu
hawezi kurithiwa na mtu yeyote yule, halafu Baba, mbona huyu msichana hata
hamlingani anaonekana ni msichana mdogo sana huoni anaweza kuwa hata mtoto wako?”
Alihoji Jamal huku akionekana kuwa na
hasira sana. Nini kinaendelea usikose sura ya ...6...
Maoni 1 :
mhhhhhh hapo patamu!jmn plsssss uwe watuwekea kila bda ya ck mbili mpz.ongera dada
Chapisha Maoni