KITABU MALIPO NI HAPAHAPA kwa wanaohitaji kutumiwa au maelekezo kukipata tuwasiliane kupitia kavisheadela@yahoo.com au +255652343430 upate kusoma simulizi ya MAMA MDOGO,,DADA YANGU NA ILIYOBEBA JINA YA KITABU MALIPO NI HAPAHAPA
ILIPOISHIA,,,,“Mama yangu! Huyu hawezi kuwa mama yangu hata siku moja. Mama yangu
hawezi kurithiwa na mtu yeyote yule, halafu baba, mbona huyu msichana hata
hamlingani anaonekana ni msichana mdogo sana huoni anaweza kuwa hata mtoto wako?”
Alihoji Jamal huku akionekana kuwa na
hasira sana.
INAPOENDELEA ,,,“Sikiliza nikwambie Jamal, mimi
ni baba yako huwezi ukanijibu maneno ya kashfa kiasi hicho. Sasa upende usipende
huyu ni mama yako kwa sababu mimi ndiye niliyeamua sawa?” Alifoka Mzee Said
huku akimwangalia Sophia.
“Mke wangu huyu ni kijana wangu anaitwa Jamal ametoka shule anaumwa sasa
hebu ni mpeleke hospitali na kesho atarudi shuleni.” Alitamka Mzee Said huku
akisimama.
“Hapana baba shule narudi muda huu sintolala hapa nina kazi nyingi za
kujisomea shuleni.” Alijibu Jamal huku akisimama na kuondoka bila hata ya
kuagana vizuri na baba yake.
“Lakini Jamal si ndio umefika
muda huu ungesubiri kidogo ili nikuandalie chakula.” Alihoji Sophia huku
akimsogelea Jamal.
Jamal aligeuka na kumtazama Sophia kisha alitoka nje bila kusema
chochote na kuondoka. Baba yake alimwita lakini Jamal alijifanya kama hasikii.
Alipofika shuleni alionekana mwingi wa mawazo, alikaa pembeni mwa mti
uliokuwa karibu na darasa alilokuwa akisoma.
“Hivi kwa nini baba ameamua kuoa hata mwaka haujaisha tangu mama
alipofariki? Isitoshe mwanamke aliyemwoa ni msichana mdogo tu? Na sidhani kama
kweli yule msichana amempenda baba yetu kwa dhati, naona kampendea hela tu. Mimi
siwezi kukubali hata kidogo, najua hizi ni mali za mama yangu mzazi, lakini kwa
sasa zipo mikononi kwa baba sijui nifanyeje.” Aliwaza sana bila kujua nini cha
kufanya.
Mwisho alifikiria kwamba hawezi kumzuia baba yake asioe kwani ameshaamua.
Kwa hiyo aliendelea na masomo yake huku akiwa anawasiliana na mdogo wake kwa
barua, lakini hakumwambia chochote kuhusu baba yake kuoa mke mwingine. Hatimaye
Jamal alimaliza mitihani ya Kidato cha Nne na kurudi nyumbani kuanza maisha
mapya.
Akiwa nyumbani baba yake alipanga kumfanyia sherehe ya kumaliza Kidato
cha Nne pindi tu mdogo wake atakaporudi kutoka shule kwani shule aliyokuwa anasoma
bado walikuwa hawajafunga. Maisha ya Jamal akiwa nyumbani yalikuwa ni ya upweke
sana, alikosa raha kila alipomwona yule mama yake mdogo na hakuwa na muda naye
hata kidogo. Sophia alijitahidi kuwa
karibu naye lakini Jamal hakutaka kabisa.
Siku moja Jamal alitoka katika matembezi na kuchelewa kurudi nyumbani,
ilikuwa ni saa tatu za usiku. Alimkuta baba yake pamoja na mama yake mdogo
wamekaa sebuleni.
“Shikamoo baba!” Aliamkia Jamal
“Umetokea wapi usiku huu, unarudi
muda unaotaka siku hizi?” Aliuliza Mzee Said kwa hasira bila hata kujibu
salamu.
“Nilikuwa na marafiki zangu samahani kwa kuchelewa.” Alijibu Jamal huku
akimuomba baba yake radhi na kuondoka.USIKOSE SURA YA ....7....
Maoni 3 :
mhhhhhhh yn yazd kunoga duh!jmn jamal mana uyo baba hashaanza kubadilika taratibu.
Haya haya simulinzi njoo utamua kolea, twipo pamoja, .........
ahhhhhhhhhhhh,adela upele umefika kwa mkunaji mbona unanikata kucha ingali upele badu upo!!!!
Chapisha Maoni