Jumatano, Juni 13, 2012

WATOTO KUTUMIKISHWA BADO NI TATIZO KUBWA TANZANIA

Jana tarehe 12 mwezi wa 6, ilikuwa ni siku ya kupiga vita vitendo vya utumikishwaji watoto.Serikali imesema asilimia 18.7 ya watoto wenye umri kuanzia miaka 5 hadi 17 bado wanatumikishwa katika ajira hatarishi nchini licha ya kuwepo kwa jitihad mbalimbali za kudhibiti vitendo hivyo.Kauli hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dk.Makongoro Mahanga.

Amesema takwimu zinaonyesha kwamba watoto hao wanatumikishwa sana katika sehemu mbalimbali kama migodini, majumbani, mashambani, katika shughuli za uvuvi na katika shughuli za ukahaba.Amesema jumla ya watoto milioni 65 wanatumikishwa katika vitendo hivyo katika nchi za Africa  zilizoko katika jangwa la Sahara, wakati watoto milioni 215 wanatumikishwa katika vitendo hivyo duniani kote.

Changamoto kubwa inayochangia vitendo hivyo ni umasikini, pamoja na utelekezaji watoto wengine kufiwa na wazazi wao au baadhi ya wazazi kuwafanya vitega uchumi vyao kwa kuwatumikisha katika shughuli za kuombaomba

Maoni 1 :

emuthree alisema ...

Hivi sijasema kitu hapa....

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom