Jumatano, Juni 13, 2012

Wivu unaua jamani "Amuua mkewe kwa wivu wa kimapenzi

Imetokea kijiji cha Mwagimagi  wilayani Geita Mkoa wa Geita Bi.Dome Shaban mwenye umri wa miaka 35 ameuawa kwa kupigwa na mumewe kwa tuhuma ya kufumaniwa akifanya ngono na mwanaume mwingine.Kamanda wa Polisi mkoani hapo amesema tukio hilo limetokea juni 11 mwaka huu majira ya saa nane usiku na kumtaja mtuhumiwa katika mauaji hayo ni Bw. Faida Anthony mwenye umri wa miaka 45 ambaye ni mume wa mwanamke huyo.

Amesema mwanamke huyo alifumaniwa akiwa na mwanaume mwingine wakifanya tendo la ngono chumbani  wakati huo mumewe hakuwepo aliporudi akagonga mlango na ndipo alipokuta mkewe akifanya mapenzi na mwanaume mwingine ambapo mwanaume aliyefumaniwa alifanikiwa kukimbia hadi sasa hajulikani jina lake na mahali anapoishi.

  Baadaye mumewe huyo alichukua kitu chenye ncha kali na kumchoma sehemu ya jicho la kulia na kushoto kabla ya kumpiga sehemu mbalimbali za mwili hali iliyosababisha kifo chake.Amesema mtuhumiwa alitoroka baada ya mauaji hayo ambapo anatafutwa na Jeshi la Polisi ili kujibu tuhuma hizo za mauaji ya mkewe

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

habari yako dada Adela, mimi natoka nje ya mada ulio iyandika mbona zile hadithi hatujajua mwisho wake ile ya MAMA MDOGO na DADA YANGU sisi wengine tupo mbali tuwekee tujue mwisho wake tumesubiri mpaka tumekata taamaa upo juu tunakupnda kwa kuwlemisha jamii

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom