Ijumaa, Juni 15, 2012

Maadhimisho Mtoto Afrika yakomeshe ukatili kwa mtoto

Siku ya mtoto Africa huadhimishwa tarehe 16 Juni ya kila mwaka kwa azimio la nchi 51 wanachama wa uliokuwa Umoja wa Nchi huru ya Africa (OAU) Kukumbuka mauaji ya kinyama waliofanyiwa watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Africa ya Kusini mwaka 1976. Siku hii huazimishwa kwa lengo la kukumbuka mauaji ya kinyama waliyofanyiwa watoto hao wakati wakidai haki zao za msingi na kuwakumbusha  wazazi na jamii juu ya haki na wajibu wa jamii katika kuwalea watoto.

 Vilevile hutoa nafasi kwa watoto kuwakumbusha haki na wajibu wao  kama watoto wa Taifa ili waweze kujua haki zao za msingi. Imesemekana bado wapo Watoto wengi ambao wamekuwa wakitumia muda mwingi wa masomo kufanya kazi za nyumbani badala ya kwenda shule hali inayoongeza idadi ya wasiojua kusoma na kuandika

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom