Mimi ni mwanamke nipo katika mahusiano ya kimapenzi na kaka mmoja ambaye tunapendana sana, tumekuwa katika mahusiano takribani miezi saba sasa, tatizo ni kwamba mimi nilishawahi kupata mtoto ambaye kwa sasa anaishi na mama yangu na sijawahi kumwambia mpenzi wangu yaani naogopa kumwambia kwa hofu ataniacha kwani alishawahi kuniambia anawashangaa sana wanaume ambao wameoa wanawake waliozalishwa nje sasa hiki kitu kinanichanganya je akifahamu na mimi nina mtoto si ataniacha naombeni ushauri nampenda sana jamani.
Maoni 4 :
SHOGA MWAMBIE KAMA KWELI ANAKUPENDA HATOKUWACHA ..NA AKIKUWACHA KUBALI MATOKEO NI MIPANGO YA MUNGU SI AJABU HAJAKUPANIG HUYO...
kama anaweza kuificha siri hiyo aendelee lakini kama hawezi ammwambie mwenzi wake ule ukweli!
Ninamfahamu mdada mwenye mtoto mwenye miaka 20 sasa alomzaa wakati wa usichana wake ambaye mumewe wa sasa ambaye wameishi naye miaka 18 lakini hajui kabisa.
Cha kuchekesha hataki huyo mwanae amwite mama wakati wowote ule bali DADA...na kijana kaachwa kwa baba yake huko kijijini shinyanga.
kesi ya huyu ni kuwa mtoto yuko kwao hapo ndo anapoona kizunguzungu!
Katika makosa makubwa ambayo wanawake wengi na hata wanaume huwa wanafanya ni kuficha kuwa na mtoto.Hilo ni jambo la kwanza kumweleza mwenzako pindi tu mnapoanza mahusiano sasa kama wewe unawaza kuvua nguo kwanza una matatizo utaishia kuchezewa.Si kosa kuwa na mtoto kwa hiyo mweke wazi ili kama yuko tayari haya mnaendelea kama hayuko tayari kila mtu anachukua 50 zake, sasa kama utamwacha akolee ndio uje kumwambia unatafuta mabalaa kwakwe na kwako.Acha kumnyanyapaa mtoto wako kwa sababu ya starehe zako.
Napita.
NAKUSHAURI UMWAMBIE TU...MTOTO NI WAKO TU HUWEZI KUKANA DAMU YAKO, LEO USIPOMTAMBULISHA UNADHANI HUYO MTOTO AKIKUA ATAJISIKIA VIZURI? WANAUME SI NDUGU ZETU ANAWEZA KUKUTENDA NA MTOTO NDO AKAWA MSAADA WAKO. MIMI PIA NILIZAA KABLA YA NDOA NA KUOLWA NA MTU MWINGINE, LAKINI NILIMFAHAMISHA MAPEMA KUWA NINA MTOTO NA KWA KUWA ANANIPENDA, HAKUONA KAMA MTOTO NI KIKWAZO....KAMA HUYO KAKA ANAKUPENDA, HATAJALI KUWA UNA MTOTO...WANASEMA UKIPENDA BOGA PENDA NA UA LAKE...SHURTI AMPENDE MWANAO.
Chapisha Maoni