Jumatano, Juni 06, 2012

NYOTA WA LEO RIHANNA

Robyn Rihanna Fenty (amezaliwa tar. 20 Februari, 1988) ni msanii wa uimbaji wa muziki wa R&B na pop kutoka nchini Barbados. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Rihanna

Alizaliwa mjini Saint Michael, Barbados, na kisha baadaye akaelekea zake nchini Marekani akiwa na umri wa miaka 16 ili kujiendeleza zaidi katika shughuli zake za kirekodi akiwa chini ya uongozi wa mtayarishaji wa rekodi Bw. Evan Rogers.

Baadaye akaja kuingia mkataba ma studio ya Def Jam Recordings baada ya kusailiwa na kiongozi wa studio hiyo Bw. Jay-Z.

Rihanna ameuza zaidi ya nakala milioni 25 za albam zake na nakala milioni 60 za single zake duniani kote tangu alipoanza fani yake mwaka 2005 ambazo zinamfanya kuwa msanii aliyeuza nakala nyingi zaidi kwa wakati wote

Mbali na kuimba msanii Rihanna pia ni muigizaji na filamu yake ya kwanza kuigiza ni "Battleship" pia ameweza kushirikiana katika filamu ya vichekesho  muvi ambayo imeongozwa na Seth Rogen namnukuu Rihanna ambaye aliandika kupitia mtandao wa twitter "Muda wa kurekodi filamu New Orleans waigizaji wote wa comedy ninaowapenda katika chumba kimoja ni vicheko kwa kwenda mbele"

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom