Mkuu wa Wilaya ya Lindi Dr Nasor Himid amesema hayo katika mazungumzo na wanachama wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF). Amesema, kawaida magari yakiwa na viyoyozi huwa na baridi ndani na inaposimama au kufunguliwa milango huingia hewa nyingine na ndipo mwili unapoweza kupata madhara amesema ni vyema kujihadhari mapema kuliko kusubiri tiba ambayo inakuwa ni gharama kubwa na wakati huohuo ubovu unakuwa umeingia mwilini.
Ukiacha tahadhari hiyo ya Mkuu wa Wilaya Wanasayansi wamewahi kutoa tahadhari kwa wanaoendesha magari wote kuwa haipaswi kufungulia kiyoyozi mara moja baada ya kuingia ndani ya gari kwa kuwa ni hatari kwa afya.
Katika taarifa mbalimbali zilizotolewa na wataalamu zimewahi kusema, Inaonyesha upo utafiti uliofanyika hivi karibuni unaonyesha kwamba kioo cha mbele cha gari hutoa kemikali ya benzene ambayo husababisha sumu iitwayo carcinogen inayosababisha saratani. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni