Jumatano, Julai 11, 2012

SIMULIZI YA MAMA MDOGO SURA YA ...9....

 KITABU MALIPO NI HAPAHAPA
MTUNZI ADELA DALLY KAVISHE

...ilipoishia.....“Hivi mimi kwanini niliolewa na huyu mzee? Nikijiangalia bado ni binti mdogo. Halafu huyu mwanawe ndo rika langu kabisa na ni mzuri sana anapendeza! Sawa nimemzidi lakini si miaka miwili au mitatu tu? Hivyo bado sisi ni rika moja kabisa! Natamani sana kuwa na kijana wa umri wa Jamal.” Aliwaza mama mdogo na kujiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu.

 
Wakati mama mdogo akiwaza ilikuwa inaelekea saa sita za mchana, alinyanyuka na kuelekea jikoni na kuandaa chakula kizuri sana. Alipika wali na kuku kisha aliandaa mezani. Wakati huo Jamal alikuwa chumbani kwake akiangalia video. Kabla ya kwenda kumwita alichukua karatasi na kuandika maneno na kuyaweka katika sahani atakayotumia Jamal. Kisha alikwenda kumwita Jamal, aliingia moja kwa moja hadi chumbani kwake.

“Vipi Jamal bado unaangalia filamu muda wa kula huu twende tukale.” Alisema mama mdogo.
“Usijali mama mdogo wewe nenda kaendelee, mimi nitakula baadaye hebu nimalizie kuangalia filamu hii.” Alijibu Jamal huku anaendelea kukodolea macho kwenye TV.
Mama yake mdogo alimsogelea na kumshika mkono.
 “Hebu twende tukale bwana mimi siwezi kula peke yangu.” Alibembeleza.
“Poa hakuna tatizo twende. Vipi na  baba anakuja kula?” Alijibu Jamal huku akivuta mkono wake.
“Baba yako alivyotingwa na kazi hawezi kuja kula mchana.” Alijibu mama mdogo.


Walipofika mezani Jamal alikaa na kuchukua sahani ndipo alipoona kikaratasi juu yake chenye ujumbe uliosomeka hivi:
“Nakupenda sana Jamal
Naomba unipe nafasi katika moyo wako,
Natamani uwe mpenzi wangu,
Naomba unijibu ni mimi Sophy.”
”Baada ya kusoma ule ujumbe Jamal alibaki ameduwaa kwa muda, kisha akamwangalia mama yake mdogo aliyekuwa amejiinamia.
“Hivi una akili kweli wewe? Yaani unaniandikia mimi ujumbe wa kimapenzi? Kama baba yangu ni mumeo mimi si mwanao? Naongea na wewe?” Alifoka Jamal huku akimtikisa kichwa mama yake mdogo.

 “Hapana baba yako ni baba yako na mimi ni mimi, kweli nakupenda Jamal tokea siku ya kwanza niliyokuona naomba tuwe pamoja tutafanya kwa siri baba yako hatajua.” Aliongea mama mdogo huku akitabasamu na kumrembulia macho Jamal.
Jamal alinyanyuka katika kiti alichokuwa amekaa kwa hasira.
“Sikiliza nikwambie we Malaya mkubwa, hata siku moja mimi siwezi kuwa na wewe. Kwanza kabisa umeolewa na baba yangu halafu unanitaka na mimi kimapenzi? Loh! Kweli wewe mwanamke ni sawa na chaja ya kobe ambayo inatumika kuchaji kila aina ya simu. Sasa kwa taarifa yako umekosea njia huwezi kunipata kwa njia yoyote ile umeniudhi sana.” Aliongea Jamal kwa jazba.

“Hata ukiniita Malaya sawa kwani najuta kuolewa na baba yako kwani hatuendani kabisa kiumri. Mimi na wewe tunaelewana kwa sababu ni rika moja nakuomba usikatae ombi langu.” Aliendelea kubembeleza mama mdogo huku akimsogelea Jamal.

 “Je, leo ndiyo unamwona baba yangu mzee? Wewe mwanamke ni muuaji naomba uniache, sikutaki na haya mambo yaishie hapa ukiendelea kunisumbua nitakuja nimwambie baba kuhusu upuuzi wako.” Alifoka Jamal na kutoka nje kwa hasira.

Mama mdogo alibaki amejiinamia katika meza akifikiria namna ya kumpata Jamal kwani mbinu ya kwanza ilishashindikana.
"Mh huyu Jamal anajidai mjanja sana kuliko mimi nitampata tu siwezi kumuacha namuhitaji sana.” Aliwaza mama mdogo huku akiondoa chakula mezani na kupeleka jikoni. haya sasa nini kitaendelea usikose SURA YA ....10,.......

Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

makubwa mama anataka kula kuku na mayai yake!lets wait n see.

emuthree alisema ...

tupo pamoja mpendwa

Bila jina alisema ...

Adela nakupenda! Cku ya kwanza tu kuja hapa nikaguna. ha ha!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom