MTUNZI ADELA DALLY KAVISHE
...ilipoishia.....“Hivi mimi kwanini niliolewa na huyu mzee? Nikijiangalia bado ni binti mdogo. Halafu huyu mwanawe ndo rika langu kabisa na ni mzuri sana anapendeza! Sawa nimemzidi lakini si miaka miwili au mitatu tu? Hivyo bado sisi ni rika moja kabisa! Natamani sana kuwa na kijana wa umri wa Jamal.” Aliwaza mama mdogo na kujiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu.
Wakati mama mdogo akiwaza ilikuwa inaelekea saa sita za mchana,
alinyanyuka na kuelekea jikoni na kuandaa chakula kizuri sana. Alipika wali na
kuku kisha aliandaa mezani. Wakati huo Jamal alikuwa chumbani kwake akiangalia
video. Kabla ya kwenda kumwita alichukua karatasi na kuandika maneno na
kuyaweka katika sahani atakayotumia Jamal. Kisha alikwenda kumwita Jamal,
aliingia moja kwa moja hadi chumbani kwake.
“Vipi Jamal bado unaangalia filamu muda wa kula huu twende tukale.”
Alisema mama mdogo.
“Usijali mama mdogo wewe nenda kaendelee, mimi nitakula baadaye hebu
nimalizie kuangalia filamu hii.” Alijibu Jamal huku anaendelea kukodolea macho
kwenye TV.
Mama yake mdogo alimsogelea na kumshika mkono.
“Hebu twende tukale bwana mimi
siwezi kula peke yangu.” Alibembeleza.
“Poa hakuna tatizo twende. Vipi na baba anakuja kula?” Alijibu Jamal huku akivuta
mkono wake.
“Baba yako alivyotingwa na kazi hawezi kuja kula mchana.” Alijibu mama
mdogo.
Walipofika mezani Jamal alikaa na kuchukua sahani ndipo alipoona
kikaratasi juu yake chenye ujumbe uliosomeka hivi:
“Nakupenda sana Jamal
Naomba unipe nafasi
katika moyo wako,
Natamani uwe mpenzi
wangu,
Naomba unijibu ni mimi
Sophy.”
”Baada ya kusoma ule ujumbe Jamal alibaki ameduwaa kwa muda, kisha akamwangalia
mama yake mdogo aliyekuwa amejiinamia.
“Hivi una akili kweli wewe? Yaani unaniandikia mimi ujumbe wa kimapenzi?
Kama baba yangu ni mumeo mimi si mwanao? Naongea na wewe?” Alifoka Jamal huku
akimtikisa kichwa mama yake mdogo.
“Hapana baba yako ni baba yako na
mimi ni mimi, kweli nakupenda Jamal tokea siku ya kwanza niliyokuona naomba
tuwe pamoja tutafanya kwa siri baba yako hatajua.” Aliongea mama mdogo huku
akitabasamu na kumrembulia macho Jamal.
Jamal alinyanyuka katika kiti alichokuwa amekaa kwa hasira.
“Sikiliza nikwambie we Malaya mkubwa, hata siku moja mimi siwezi kuwa na
wewe. Kwanza kabisa umeolewa na baba yangu halafu unanitaka na mimi kimapenzi?
Loh! Kweli wewe mwanamke ni sawa na chaja ya kobe ambayo inatumika kuchaji kila
aina ya simu. Sasa kwa taarifa yako umekosea njia huwezi kunipata kwa njia
yoyote ile umeniudhi sana.” Aliongea Jamal kwa jazba.
“Hata ukiniita Malaya sawa kwani najuta kuolewa na baba yako kwani
hatuendani kabisa kiumri. Mimi na wewe tunaelewana kwa sababu ni rika moja
nakuomba usikatae ombi langu.” Aliendelea kubembeleza mama mdogo huku
akimsogelea Jamal.
“Je, leo ndiyo unamwona baba
yangu mzee? Wewe mwanamke ni muuaji naomba uniache, sikutaki na haya mambo
yaishie hapa ukiendelea kunisumbua nitakuja nimwambie baba kuhusu upuuzi wako.”
Alifoka Jamal na kutoka nje kwa hasira.
Mama mdogo alibaki amejiinamia katika meza akifikiria namna ya kumpata
Jamal kwani mbinu ya kwanza ilishashindikana.
"Mh huyu Jamal anajidai mjanja sana kuliko mimi nitampata tu siwezi
kumuacha namuhitaji sana.” Aliwaza mama mdogo huku akiondoa chakula mezani na
kupeleka jikoni. haya sasa nini kitaendelea usikose SURA YA ....10,.......
Maoni 3 :
makubwa mama anataka kula kuku na mayai yake!lets wait n see.
tupo pamoja mpendwa
Adela nakupenda! Cku ya kwanza tu kuja hapa nikaguna. ha ha!
Chapisha Maoni